

Lugha Nyingine
China yaikemea Marekani juu ya vizuizi vipya vya uwekezaji, yaapa kulinda maslahi yake
BEIJING - Kwa kufungia mlango kampuni za China na soko la China, Marekani itaishia kuumiza maslahi yake ya kiuchumi na kuaminika kwake duniani, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Lin Jian amesema Jumatatu.
Lin ametoa kauli hiyo kwenye mkutano na wanahabari alipokuwa akitoa maoni kuhusu waraka uliotolewa na Marekani siku ya Ijumaa, ambao umebainisha vizuizi zaidi vya uwekezaji wa pande mbili na China.
Waraka huo umeiorodhesha China kama "adui wa kigeni" kwa misingi ya usalama wa taifa na kuweka hatua mbalimbali za kibaguzi, Lin amesema. "Tunalaani sana na tunapinga kwa dhati hili na tumewasilisha malalamiko yetu kwa Marekani" ameeleza.
Amesema, kubanisha ukaguzi wa kiusalama unaolenga uwekezaji wa China nchini Marekani kunaathiri vibaya sana imani ya kampuni za China katika kuwekeza nchini Marekani na kudhoofisha mazingira ya biashara ya Marekani.
Aidha, Lin amesema kuwa, kuongeza vizuizi kwa uwekezaji wa Marekani nchini China kunaingilia kiholela maamuzi huru ya kampuni za Marekani, na kumeharibu mawasiliano ya uwekezaji kati ya nchi hizo mbili.
"China inaitaka Marekani kutii sheria za kimataifa za uwekezaji na biashara, kuheshimu sheria za uchumi wa soko, na kuacha kuingiza mambo ya siasa au kutumia masuala ya kiuchumi na kibiashara kama silaha," amesema msemaji huyo.
“China pia inaitaka Marekani kuacha kuhujumu haki halali za maendeleo ya China,” ameongeza Lin, akisisitiza kuwa China itachukua hatua zote stahiki kulinda kithabiti haki na maslahi yake halali.
Wakati akijibu kuhusu vizuizi vya Marekani kwa sekta ya utegenezaji wa meli ya China na sekta nyingine zinazohusiana, Lin amesema kuwa Marekani, ikiendeshwa na maslahi yake ya kisiasa ya ndani, imetumia vibaya utaratibu wa uchunguzi wa Kifungu cha 301, na hivyo kukiuka kwa kiasi kikubwa sheria za WTO na kuharibu zaidi mfumo wa biashara wa pande nyingi. "China inaeleza kutoridhika sana na hili na inapinga vikali," Lin amesema.
"Tunaitaka Marekani kuheshimu ukweli na sheria za pande nyingi, na kuacha mara moja vitendo vyake potofu. China itachukua hatua ili kulinda haki na maslahi yake halali," Lin ameongeza.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma