Rais Xi asema uhusiano wa pande mbili unaonyesha China na Russia ni majirani wazuri, marafiki wa kweli

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 25, 2025

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na Rais wa Russia Vladimir Putin kutokana na ombi la rais huyo wa Russia Februari 24, ambapo amesema kuwa historia na hali halisi ya hivi sasa zinaonyesha kuwa China na Russia ni majirani wema ambao hawawezi kuhamishwa, na ni marafiki wa kweli katika hali ya dhiki na faraja, ambao wanaungana mkono na kupata maendeleo kwa pamoja.

Rais Xi amesema viongozi hao wawili walifanya mkutano kwa njia ya video kabla ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China ambapo walipanga mipango ya maendeleo ya uhusiano kati ya China na Russia katika mwaka mzima na kuimarisha uratibu katika mfululizo wa masuala makubwa ya kimataifa na kikanda.

Rais Xi amesema, "Idara mbalimbali za nchi zetu mbili zinahimiza kwa hatua madhubuti ushirikiano katika sekta mbalimbali kwa kufuata makubaliano tuliyofikia sisi wawili, ikiwemo kufanya shughuli za kuadhimisha miaka 80 ya ushindi wa Vita vilivyofanywa na Watu wa China vya kupambana na Uvamizi wa Japan na maadhimisho ya miaka 80 ya ushindi wa Vita vya Dunia vya Kupambana na Ufashisti."

Rais Xi amesema uhusiano kati ya China na Russia una msukumo mkubwa kutokana na nguvu ya ndani na thamani ya kipekee ya kimkakati, akiongeza kuwa uhusiano huo haulengi upande wowote wa tatu wala hautaathiriwa na upande wowote wa tatu. Amesema, mikakati ya maendeleo na sera za nje za China na Russia ni kwa ajili ya muda mrefu.

“Bila ya kujali mabadiliko ya namna gani yakitokea katika hali ya kimataifa, uhusiano kati ya China na Russia utaendelea kwa utulivu, ambao utasaidia maendeleo na ustawishaji wa kila mmoja, na kuleta utulivu na nishati chanya katika uhusiano wa kimataifa,” amesema.

Rais Xi amesisitiza kwamba mwanzoni mwa kupamba moto pande zote kwa mgogoro wa Ukraine, alitoa mapendekezo "manne-yanayopaswa" na mapendekezo mengine ya msingi ya kutatua mgogoro huo.

“China inafurahia Russia na pande husika zikifanya juhudi za kuondoa msukosuko, ” amesema.

Kwa upande wake, Rais Putin amesema Russia inatilia maanani sana uhusiano wake na China na inatarajia kudumisha mawasiliano kwenye ngazi ya juu na China katika Mwaka Mpya, kuzidisha ushirikiano wa kivitendo, na kuadhimisha kwa pamoja miaka 80 ya ushindi wa Vita vya Dunia vya Kupambana na Ufashisti na ushindi wa Vita vilivyofanywa na Watu wa China vya kupambana na Uvamizi wa Japan.

“Kuendeleza uhusiano na China ni chaguo la kimkakati lililofanywa na Russia kwa mtazamo wa muda mrefu, badala ya hatua ya kutumiana kimaslahi,” Rais Putin amesema, akiongeza kuwa mkakati huo hauathiriwi na mwelekeo wowote wa muda mfupi au usumbufu wa nje.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha