

Lugha Nyingine
Makadirio ya matokeo ya mwisho yaonesha vyama vya kihafidhina vya CDU/CSU kuongoza katika uchaguzi wa Ujerumani
Friedrich Merz, mwenyekiti wa chama cha Christian Democratic Union (CDU) cha Ujerumani, akipiga kura kwenye kituo cha kupigia kura mjini Arnsberg, Ujerumani, Februari 23, 2025. (Xinhua/Zhang Fan)
BERLIN - Muungano wa vyama vya kihafidhina vya Ujerumani, Christian Democratic Union (CDU) na Christian Social Union (CSU), umechukua uongozi katika uchaguzi mkuu wa Ujerumani mwaka 2025, kwa mujibu wa makadirio ya kura za maoni ya watu waliokuwa wakitoka vituoni kupiga kura yaliyotolewa na shirika la utangazaji la ARD jana Jumapili jioni.
Kura hiyo ya maoni inaonyesha kuwa vyama vya CDU na CSU vimepata asilimia 29 ya kura, vikifuatiwa na chama cha Alternative for Germany (AfD) kilichopata asilimia 19.5 na Social Democratic Party (SPD) kilichopata asilimia 16.
Chama cha The Greens kimeshika nafasi ya nne kwa kupata asilimia 13.5 ya kura, mbele ya chama cha Die Linke kikipata asilimia 8.5 ya kura.
Friedrich Merz, mwenyekiti wa chama cha Christian Democratic Union (CDU) cha Ujerumani, akipiga kura kwenye kituo cha kupigia kura mjini Arnsberg, Ujerumani, Februari 23, 2025. (Xinhua/Zhang Fan)
Vyama vya Free Democratic Party (FDP) na Muungano wa Sahra Wagenknecht (BSW) vinakadiwa vitapata asilimia 4.9 na 4.7 ya kura mtawalia.
Uchaguzi huo utaamua muundo wa bunge lijalo la Ujerumani, Bundestag, baraza la chini la bunge la Ujerumani.
Bunge hilo jipya lililochaguliwa litamchagua chansela ajaye wa Ujerumani kufuatia majadiliano ya miungano kati ya vyama ili kuunda serikali ya mseto.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma