Roboti ya muundo wa mbwa ya China yavutia watu kwa burudani kwenye Maonesho ya Vyombo vya Habari ya Saudi Arabia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 21, 2025

Watu wakitazama burudani ya roboti ya muundo wa mbwa iliyozalishwa na kampuni ya China, Unitree Robotics, kwenye Maonesho ya Mustakabali wa Vyombo vya Habari mjini Riyadh, Saudi Arabia, Februari 20, 2025. (Xinhua/Yin Ke)

Roboti ya muundo wa mbwa ya China imevutia watazamaji kwa mijongeo yake ya kucheza dansi kwenye Maonesho ya Mustakabali wa Vyombo vya Habari, ambayo yanafanyika sambamba na Jukwaa la Vyombo vya Habari la Saudi Arabia ambalo lilianza Jumatano na litafikia tamati leo Ijumaa jijini Riyadh.

Mbali na kucheza dansi, roboti hiyo ya muundo wa mbwa huwasiliana na watazamaji kwa ishara mbalimbali, ikiruka, kujinyoosha, kushikana mikono, kushangilia, kuruka, na kutulia chini kwa mikogo. Watazamaji wanaovutiwa huchukua simu zao haraka ili kurekodi burudani hiyo, wakizunguka zunguka kwa muda mrefu mbele ya banda hilo.

"Mbwa mwerevu kiasi hiki!" mwanablogu kutoka Bahrain alishangaa baada ya roboti hiyo kuonyesha ishara ya "moyo wa kidole" kwa ustadi. "Nitachapisha video hii kwenye mitandao ya kijamii."

Akiwa amepewa jina la Go2 Pro, mbwa huyo roboti ni toleo jipya kabisa lililotolewa na kampuni ya China, Unitree Robotics, mwaka 2023. Ikiwa na rada ya kisasa ya laser ya 4D LIDAR L1 iliyotengenezwa na Unitree yenyewe, roboti hiyo yenye miguu minne ina sifa za utambuzi mpana mkubwa, sehemu chache zisizoonekana, kuhisi vitu vilivyo karibu kwa umbali hadi mita 0.05, na kuhimili mazingira mbalimbali ya ardhi.

"Roboti za miguu minne zinazotengenezwa na Unitree zinatumika zaidi katika utafiti, ukaguzi, na udhibiti wa moto," zinapokuwa zimewekewa vifaa mbalimbali, Wang Xinyi, meneja wa mauzo wa Unitree katika eneo la Mashariki ya Kati, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua, akibainisha kuwa roboti hizo za miguu minne za Unitree kwa sasa zinachukua asilimia 60 hadi 70 ya mauzo ya roboti za aina hiyo duniani.

Watu wakitazama burudani ya roboti ya muundo wa mbwa iliyozalishwa na kampuni ya China, Unitree Robotics, kwenye Maonesho ya Mustakabali wa Vyombo vya Habari mjini Riyadh, Saudi Arabia, Februari 20, 2025. (Xinhua/Yin Ke)

Watu wakitazama burudani ya roboti ya muundo wa mbwa iliyozalishwa na kampuni ya China, Unitree Robotics, kwenye Maonesho ya Mustakabali wa Vyombo vya Habari mjini Riyadh, Saudi Arabia, Februari 20, 2025. (Xinhua/Yin Ke)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha