Kremlin yaeleza wasiwasi juu ya mipango ya kutumwa wanajeshi wa NATO nchini Ukraine

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 21, 2025
Kremlin yaeleza wasiwasi juu ya mipango ya kutumwa wanajeshi wa NATO nchini Ukraine
Picha hii iliyopigwa Februari 7, 2024 ikionyesha mwonekano wa majira ya baridi ya Ikulu ya Russia, Kremlin mjini Moscow, Russia. (Xinhua/Cao Yang)

MOSCOW - Mipango yenye uwezekano wa kupeleka vikosi vya Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi (NATO) nchini Ukraine inatia wasiwasi, msemaji wa Ikulu ya Russia, Kremlin Dmitry Peskov amesema jana Alhamisi kufuatia ripoti kwamba Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer anatazamiwa kupendekeza kwa Rais wa Marekani Donald Trump mpango wa kulinda amani nchini Ukraine, ambao unatarajiwa kutuma wanajeshi hadi 30,000 wa Ulaya katika miji ya Ukraine.

Peskov amesema Moscow imekuwa ikifuatilia kwa karibu taarifa zote zinazotolewa na maafisa wa Ulaya.

"Hili ni suala la wasiwasi kwetu ... kwa kuwa tunajadili uwezekano wa kutumwa kwa vikosi vya kijeshi kutoka nchi za NATO nchini Ukraine," Peskov amesema.

Pia amesema kwamba malengo yote nchini Ukraine yanapasa kufikiwa kwa njia za amani, akiongeza kuwa serikali ya Trump unaamini kuwa ni muhimu kupatikana kwa amani mapema iwezekanavyo kupitia majadiliano, na kwamba Moscow inakubaliana sana na njia hii.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha