

Lugha Nyingine
China yachukua nafasi ya pili duniani katika nguvu laini za ushawishi
(CRI Online) Februari 21, 2025
China imekuwa nchi ya pili kwa kuwa na ushawishi mkubwa duniani katika nguvu laini baada ya Marekani, kwa mujibu wa ripoti ya 6 ya mwaka ya Viwango vya Nguvu Laini ya Ushawishi Duniani Mwaka 2025 iliyotolewa jana Alhamisi jijini London, Uingereza na Brand Finance.
Marekani inaendelea kuchukua nafasi ya kwanza, huku Uingereza, Japan na Ujerumani zikichukua nafasi za tatu hadi tano.
Ripoti hiyo imesema, ongezeko la nguvu laini ya ushawishi wa China inatokana na China kuhimiza utekelezaji wa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, kuimarisha maendeleo endelevu, na kuongezeka kwa nguvu ya chapa za nchi hiyo.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma