

Lugha Nyingine
Mabaki ya mwili wa Naibu Waziri Mkuu wa Zamani wa China Zou Jiahua yachomwa Beijing
Rais Xi Jinping wa China akipeana mkono na mwanafamilia wa Zou Jiahua kutoa salamu za rambirambi mjini Beijing, China, Februari 20, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)
BEIJING - Mabaki ya mwili wa Zou Jiahua, naibu waziri mkuu wa zamani wa China, yamechomwa moto Beijing jana Alhamisi ambapo Rais Xi Jinping wa China pamoja na viongozi wengine wa Chama na serikali wakiwemo Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang, Li Xi na Han Zheng, wamemuaga Zou kwenye Makaburi ya Wanamapinduzi ya Babaoshan asubuhi ya siku hiyo.
Zou alifariki Februari 16 mjini Beijing akiwa na umri wa miaka 99.
Huku kukiwa na muziki wa maombolezo, viongozi hao walitembea polepole kuelekea kwenye jeneza la mwili wa Zou na kusimama kwa utulivu kumkumbuka. Kisha wakatoa heshima zao za mwisho kwa kuinamia mara tatu kwa mwili wake, wakapeana mikono na familia ya Zou na kutoa rambirambi.
Zou alikuwa mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya 14 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na naibu mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la tisa la Umma la China.
Alisifiwa kuwa mwanachama bora wa CPC, mpiganaji mtiifu wa kikomunisti aliyejaribiwa kwa muda, mwanamapinduzi wa tabaka la wafanyakazi, na ni kiongozi bora katika kuhimiza maendeleo ya uchumi wa China na viwanda vya ulinzi wa taifa, na kuhimiza kuendeleza mambo ya mfumo wa kisheria wa kijamaa.
Xi Jinping, Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang, Li Xi, Han Zheng na Hu Jintao ama walimtembelea Zou alipokuwa hospitalini, au wamemuomboleza na kutuma salamu za rambirambi kwa familia yake kupitia njia mbalimbali kufuatia kifo chake.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma