

Lugha Nyingine
Ufaransa yakabidhi rasmi kambi ya kijeshi ya Port Boué kwa Cote d'Ivoire
(CRI Online) Februari 21, 2025
Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Sébastien Lecornu na Waziri wa Ulinzi wa Cote d'Ivoire Téné Birahima Ouattara kwa pamoja wamesaini hati ya makabidhiano jana Alhamisi katika Bandari ya Bouet mjini Abidjan, ambapo Ufaransa imekabidhi rasmi kituo cha kijeshi cha Bandari ya Bouet kwa Cote d'Ivoire.
Mapema siku hiyo, Ufaransa kwanza ilikabidhi kambi ya Kikosi cha 43 cha Wanamaji wa Ufaransa, ambayo awali ilikuwa kwenye kituo cha kijeshi cha Bandari ya Bouet, kwa jeshi la Cote d'Ivoire.
Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya nchi hiyo, Côte d'Ivoire itakipa kituo hicho cha kijeshi cha Port Bouet jina la Mnadhimu Mkuu wa kwanza jeshi la nchi hiyo baada ya uhuru wake.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma