Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa afanya ziara nchini Kenya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 20, 2025

Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA ) Philemon Yang akitoa hotuba ya kufanya majumuisho kwenye Mjadala wa kawaida wa mkutano wa Baraza Kuu la 79 la Umoja wa Mataifa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Septemba 30, 2024. (Xinhua/Li Rui)

Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) Philemon Yang akitoa hotuba ya kufanya majumuisho kwenye Mjadala wa kawaida wa mkutano wa 79 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Septemba 30, 2024. (Xinhua/Li Rui)

NAIROBI - Mwenyekiti wa Mkutano wa 79 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN) Philemon Yang ameanza ziara ya siku nne nchini Kenya siku ya Jumanne ili kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hiyo na shirika hilo la kimataifa, serikali ya Kenya imetangaza.

Wizara ya Mambo ya Nje na Masuala ya Diaspora ya Kenya imesema kuwa ziara hiyo ya Yang itaimarisha kazi muhimu ya nchi hiyo katika mambo ya diplomasia ya pande nyingi na ahadi yake katika kuhimiza mambo muhimu ya kimatafia na kikanda yanayopewa vipaumbele.

"Ziara hii itadhihirisha ushirikiano imara na wa kudumu kati ya Kenya na Umoja wa Mataifa, na kuunga mkono uongozi wa Kenya katika masuala ya kikanda na kimataifa," wizara hiyo imesema katika taarifa yake iliyotolewa Nairobi, Kenya.

Rais wa Kenya William Ruto akizungumza kwenye mahojiano na Shirika la Habari la China, Xinhua mjini Nairobi, Kenya Agosti 26, 2024. (Xinhua/Han Xu)

Rais wa Kenya William Ruto akizungumza kwenye mahojiano na Shirika la Habari la China, Xinhua mjini Nairobi, Kenya Agosti 26, 2024. (Xinhua/Han Xu)

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, wakati wa ziara yake hiyo, Yang amepanga kukutana na Rais wa Kenya William Ruto na maofisa wengine waandamizi wa serikali, ambapo ataeleza matarajio yake na mambo yatakayopewa vipaumbele katika kipindi chake cha uongozi. Majadiliano yataweka mkazo katika amani na usalama, maendeleo endelevu, kuendeleza kazi ya kukusanya mitaji, maendeleo ya kidigitali, na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa.

Yang pia atatoa mhadhara wa umma na kuzungumza na wafanyakazi wa jumuiya ya Umoja wa Mataifa, wasomi, taasisi za washauri bingwa wa sera, wavumbuzi, na wadau wa sekta binafsi. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha