Viongozi wa Ulaya wasisitiza wito wa amani ya haki na ya kudumu nchini Ukraine

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 20, 2025

Bendera za Umoja wa Ulaya zikipepea nje ya Jengo la Berlaymont, makao makuu ya Kamisheni ya Ulaya, mjini Brussels, Ubelgiji, Januari 29, 2025. (Xinhua/Meng Dingbo)

Bendera za Umoja wa Ulaya zikipepea nje ya Jengo la Berlaymont, makao makuu ya Kamisheni ya Ulaya, mjini Brussels, Ubelgiji, Januari 29, 2025. (Xinhua/Meng Dingbo)

PARIS - Kufuatia mazungumzo kati ya Russia na Marekani yaliyofanyika juzi Jumanne mjini Riyadh, Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ameitisha mkutano wa pili juu ya Ukraine na usalama wa Ulaya jana siku ya Jumatano, akiwakutanisha pamoja washirika wa Ufaransa wa Ulaya na wasio wa Ulaya.

Tofauti na mkutano mdogo wa kilele wa ana kwa ana uliofanyika mapema siku ya Jumatatu wiki hii, Macron amekuwa na "mazungumzo marefu" kupitia mkutano huo wa jana uliofanyika kwa njia ya video na wenzake wa Umoja wa Ulaya (EU) na viongozi kutoka Norway, Iceland, na Canada. Rais wa mpito wa Romania Ilie Bolojan pia alialikwa na kufanya mazungumzo ya pande mbili na Macron kabla ya mkutano huo.

Baada ya mkutano huo, viongozi wa Ulaya wamesisitiza msimamo wao kwamba amani "ya haki na ya kudumu" nchini Ukraine lazima ipatikane. Macron ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X kwamba msimamo wa Ufaransa na washirika wake kuhusu Ukraine uko "wazi na wenye umoja."

"Tunataka amani ya kudumu na thabiti nchini Ukraine," Macron amesisitiza, akiongeza kuwa nchi za Ulaya zitasimama na Ukraine na "tutabeba wajibu wetu wote kuhakikisha amani na usalama barani Ulaya."

Macron amesisitiza kuwa Ulaya ina lengo sawa na Rais wa Marekani Donald Trump -- kumaliza mgogoro huo uliodumu kwa miaka mitatu nchini Ukraine.

Amesisitiza kwamba juhudi za Ulaya kwa ajili ya amani zitaendelea chini ya kanuni tatu: Ukraine lazima ishirikishwe na haki zake kuheshimiwa, amani lazima iwe ya kudumu na iambatane na dhamana thabiti na za uhakika, na ufuatiliaji wa Ulaya juu ya amani lazima utiliwe maanani.

Akiwa ni afisa pekee aliyepokelewa na Macron katika Ikulu ya Elysee jijini Paris siku hiyo ya Jumatano, Rais wa mpito wa Romania Ilie Bolojan ameunga mkono maoni hayo ya Macron, akisisitiza kuwa amani ya "haki na usawa" ni muhimu na haiwezi kufikiwa bila ushiriki wa Ukraine na EU.

Picha hii iliyopigwa Mei 22, 2024 ikionyesha Ikulu ya White House mjini Washington, D.C., Marekani. (Xinhua/Liu Jie)

Picha hii iliyopigwa Mei 22, 2024 ikionyesha Ikulu ya White House mjini Washington, D.C., Marekani. (Xinhua/Liu Jie)

Viongozi wengine wa Ulaya wakiwemo, Waziri Mkuu wa Sweden Ulf Kristersson, Waziri Mkuu wa Croatia Andrej Plenkovic, Waziri Mkuu wa Norway Jonas Gahr Store, Rais wa Finland Alexander Stubb na Waziri Mkuu Petteri Orpo pia wametoa misimamo yanayofanana baada ya kuhudhuria mkutano huo kwa njia ya video.

Picha hii iliyopigwa Desemba 20, 2024 ikionyesha uharibifu uliosababishwa na shambulizi la kombora na droni la Russia mjini Kiev, Ukraine. (Picha na Roman Petushkov/Xinhua)

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Baltic (BNS), Rais wa Lithuania Gitanas Nauseda amependekeza kuiteua Januari 1, 2030 kuwa "tarehe rejea" kwa Ukraine kujiunga rasmi na EU. Mapema kabla ya mkutano huo, Nauseda alitoa wito wa kuungwa mkono bila masharti kwa Ukraine na kuongeza matumizi katika ulinzi na usalama.

"Hakuna majadiliano juu ya Ukraine bila Ukraine, hakuna majadiliano juu ya Ulaya bila Ulaya," amesema.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha