

Lugha Nyingine
Waziri wa Mambo ya Nje wa China ahimiza China na Marekani kutafuta njia sahihi ya kutendeana
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akifanya mazungumzo na wajumbe wa sekta mbalimbali za Marekani katika wakati wa kuhudhuria mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mjini New York, Februari 18, 2025. (Xinhua/Li Rui)
UMOJA WA MATAIFA - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) katika mazungumzo na wajumbe wa sekta mbalimbali za Marekani siku ya Jumanne katika wakati wa kuhudhuria mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mjini New York, amesema kuwa China na Marekani zinapaswa kutafuta njia sahihi ya kutendeana.
Wang amesema China na Marekani zinapaswa kufuata kanuni za kuheshimiana, kuishi pamoja kwa amani na kufanya ushirikiano wa kunufaisha, na kutafuta njia sahihi kwa nchi hizo mbili kubwa kutendeana kirafiki.
Wang, amesema kuwa China na Marekani zina maslahi makubwa ya pamoja na kuna nafasi pana kwa ushirikiano.
"Kila upande wa pande hizo mbili unapaswa kuheshimu kihalisi maslahi ya kimsingi ya upande mwingine, kuimarisha mawasiliano, kujenga hali ya kuaminiana, kuzuia mambo yenye kuvuruga na kushinda vizuizi ili uhusiano kati ya China na Marekani uweze kuboreshwa na kupata utulivu,” amesema Wang.
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akifanya mazungumzo na wajumbe wa sekta mbalimbali za Marekani huko New York, Februari 18, 2025. (Xinhua/Li Rui)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma