Morocco na Ufaransa zatia saini makubaliano ya kuimarisha ushirikiano wa kitamaduni

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 19, 2025

Waziri wa Vijana, Utamaduni na Mawasiliano wa Morocco Mohamed Mehdi Bensaid (Kulia) na Waziri wa Utamaduni wa Ufaransa Rachida Dati wakihudhuria hafla ya kutia saini makubaliano ya kitamaduni kati ya Morocco na Ufaransa mjini Rabat, Morocco, Februari 18, 2025. (Xinhua/Huo Jing)

RABAT - Morocco na Ufaransa zimetia saini makubaliano kadhaa mjini Rabat, mji mkuu wa Morocco ili kuimarisha ushirikiano wa kitamaduni kuhusu filamu, akili mnemba, ulinzi wa urithi wa kitamaduni, na uendelezaji wa michezo ya video.

Hafla hiyo ya utiaji saini imefanyika jana Jumanne, siku ya mwisho ya ziara ya kikazi ya siku tatu ya Waziri wa Utamaduni wa Ufaransa Rachida Dati.

Kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo, Waziri wa Vijana, Utamaduni na Mawasiliano wa Morocco Mohamed Mehdi Bensaid amesifu ushirikiano na uhusiano wa kiwenzi kati ya nchi hizo mbili.

Amesisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya sekta binafsi za nchi zote mbili, haswa katika nyanja ibuka kama vile michezo ya video.

Kwa upande wake Dati amesema kwenye mkutano huo na waandishi wa habari kwamba uhusiano wa kitamaduni ni "nguzo katika msingi wa siku za baadaye" kwa uhusiano kati ya Ufaransa na Morocco na kuelezea nia ya Ufaransa kuwa mshirika wa Morocco katika mkakati wake wa kitamaduni wa kimataifa. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha