Marekani na Russia zakubaliana kuboresha uhusiano na kufanya juhudi katika kumaliza mgogoro wa Ukraine

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 19, 2025

Picha hii iliyopigwa Desemba 20, 2024 ikionyesha uharibifu uliosababishwa na shambulizi la kombora na droni la Russia mjini Kiev, Ukraine. (Picha na Roman Petushkov/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Desemba 20, 2024 ikionyesha uharibifu uliosababishwa na shambulizi la kombora na droni la Russia mjini Kiev, Ukraine. (Picha na Roman Petushkov/Xinhua)

RIYADH - Marekani na Russia zimekubaliana kufanya juhudi kwa ajili ya kumaliza mgogoro nchini Ukraine na kuboresha uhusiano kati ya pande hizo mbili wakati wa mazungumzo ya kina ya ngazi ya juu yaliyofanyika Riyadh, Saudi Arabia jana Jumanne.

Kwenye mazungumzo hayo ya kwanza ya ana kwa ana kati ya maafisa waandamizi wa Marekani na Russia tangu kuzuka kwa mgogoro huo kati ya Russia na Ukraine Februari 2022, ujumbe wa Russia, ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Sergei Lavrov na mshauri wa mambo ya nje wa Kremlin Yuri Ushakov, wamekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio, ambaye aliambatana na Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani Mike Waltz na Mjumbe Maalum wa Mashariki ya Kati wa Marekani Steve Witkoff.

Mwanajeshi wa kikosi cha bunduki zinazoendeshwa kwenye gari cha brigedi ya 93 akionyesha bunduki ya kukinga droni mjini Donetsk, Ukraine, Agosti 15, 2024. (Picha na Peter Druk/Xinhua)

Majadiliano mazito

Kufuatia mazungumzo hayo yaliyodumu kwa saa nne na nusu, Witkoff ameyaelezea mazungumzo ya Riyadh kuwa ni "chanya, ya kusisimua, ya kiujenzi."

Ushakov amesema ilikuwa "majadiliano mazito sana kuhusu masuala yote tunayotaka kuyagusia," akibainisha kuwa pande hizo mbili zimekubaliana kutilia maanani maslahi ya kila upande na kuendeleza uhusiano wa pande mbili.

Marekani na Russia zimekubaliana "kuanzisha utaratibu wa mashauriano kushughulikia mambo yanayokera katika uhusiano wetu wa pande mbili kwa lengo la kuchukua hatua hitajika ili kurejesha kawaida kazi za balozi zetu za kidiplomasia," kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.

Washington na Moscow "zitateua timu husika za ngazi ya juu kutafuta njia ya kumaliza mgogoro nchini Ukraine haraka iwezekanavyo kwa njia ambayo ni ya kudumu, endelevu, na inayokubalika kwa pande zote," imesema taarifa hiyo.

Kwenye mkutano na waandishi wa habari kufuatia mkutano huo, Lavrov ameyaelezea mazungumzo hayo kuwa "ya manufaa sana," akisisitiza msimamo thabiti wa Russia kwamba kutumwa kwa wanajeshi wa NATO nchini Ukraine ni jambo lisilokubalika.

Askari wa zima moto wakijaribu kuzima moto kwenye jengo mjini Donetsk, Ukraine, Agosti 5, 2023. (Picha na Victor/Xinhua)

Maoni tofauti

Baada ya mgogoro huo mkubwa kati ya Russia na Ukraine kuzuka, serikali ya Marekani chini ya utawala wa Joe Biden ilichukua msimamo thabiti pamoja na washirika wake wa Ulaya, ikitoa uungaji mkono wake kamili nyuma ya Ukraine kwa kutoa msaada mkubwa wa kijeshi na kuitenga Russia katika jukwaa la kimataifa.

Linapokuja suala la uwezekano wa mazungumzo kati ya Russia na Ukraine, msimamo ambao hapo awali wa Marekani na Ulaya ulikuwa "hakuna mazungumzo yoyote kuhusu Ukraine bila Ukraine," ukisisitiza nafasi kuu ya Ukraine katika mazungumzo yoyote yajayo.

Mabadiliko ya msimamo huo wa Marekani kuhusu mgogoro kati ya Ukraine na Russia yanatokea huku kukiwa na hali ya kuongezeka kwa tofauti katika uelewa wa ushirikiano wa kiulinzi kati ya Marekani na Ulaya.

Washington imekuwa ikielezea mara kwa mara kutoridhishwa na washirika wake hao wa Ulaya kwa kutotoa wajibu wao katika matumizi ya ulinzi.

Wakati huo huo, baadhi ya viongozi wa Ulaya akiwemo Rais wa Ukraine mwenyewe Volodymyr Zelensky wameelezea kusikitika kwao kutokana na kutengwa kwao katika mazungumzo hayo kati ya Marekani na Russia.

Kufuatia mkutano huo wa Riyadh, Rais Zelensky, ambaye alikuwa ziarani nchini Uturuki (wakati habari hii inaripotiwa), amesema kuwa mazungumzo kati ya Russia na Marekani ni "mshangao" kwa Kiev, ambayo "imekuja kuyafahamu kupitia vyombo vya habari."

Picha ya skrini ya video iliyotolewa na Wizara ya Hali ya Dharura ya Russia ikionyesha waokoaji wakifanya kazi kwenye eneo lililoshambuliwa kwa makombora katika Mji wa Lysychansk katika Mkoa wa Lugansk, Februari 3, 2024. (Xinhua)

Picha ya skrini ya video iliyotolewa na Wizara ya Hali ya Dharura ya Russia ikionyesha waokoaji wakifanya kazi kwenye eneo lililoshambuliwa kwa makombora katika Mji wa Lysychansk katika Mkoa wa Lugansk, Februari 3, 2024. (Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha