

Lugha Nyingine
China yapeleka misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza kupitia Jordan
Malori yaliyopakiwa vitu vya msaada wa China yakijiandaa kuondoka kwenye ghala la Shirika la Hisani la Hashemite la Jordan huko Zarqa, Jordan, Februari 18, 2025. (Picha na Mohammad Abu Ghosh/Xinhua)
AMMAN - Ubalozi wa China nchini Jordan na Shirika la Hisani la Hashemite la Jordan zimefanya hafla ya kuondoka kwa shehena ya vitu vya msaada wa kibinadamu uliotolewa na China hadi katika Ukanda wa Gaza wa Palestina.
Vitu vya msaada huo wa dharura wa kibinadamu vitasafirishwa kutoka Jordan hadi Gaza kupitia mipaka ya nchi kavu. Vitu vya maboksi 60,000 vya chakula, na vitawasilishwa katika shehena sita.
Shehena ya kwanza yenye vifurushi 12,000 vya chakula, itakabidhiwa kwa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, Shirika la Hilali Nyekundu la Palestina, na mashirika mengine husika mara itakapofika Gaza.
Kwenye hafla hiyo, Balozi wa China nchini Jordan Chen Chuandong amesema kuwa, China ikiwa ni rafiki wa watu wa Palestina, imetoa vitu vingi vya msaada kwa Ukanda wa Gaza, na itaendelea kutoa msaada kwa watu wa Palestina.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Shirika la Hisani la Hashemite Hussein Shibli ametoa shukrani zake kwa China kwa uungaji mkono wake kwa wakazi wa Gaza, akielezea matumaini yake kwa ushirikiano zaidi na China katika siku zijazo kusaidia wale wenye mahitaji katika ukanda huo.
Mfanyakazi akiandaa lori lililopakiwa vitu vya msaada wa China kwenye ghala la Shirika la Hisani la Hashemite la Jordan mjini Zarqa, Jordan, Februari 18, 2025. (Picha na Mohammad Abu Ghosh/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma