

Lugha Nyingine
Jeshi la China laonya ndege ya Ufilipino kuruka kutoka anga ya mamlaka ya China juu ya Kisiwa cha Huangyan
GUANGZHOU –Msemaji wa jeshi la China amesema Jumanne iliyopita kuwa, Vikosi vya majeshi ya majini na angani vya Eneo la Kivita la Kusini la Jeshi la Ukombozi wa Umma la China, kwa mujibu wa sheria na kanuni, vimeibainisha, kuifuatilia, na kuonya ndege ya Ufilipino C-208 kuruka kutoka anga ya mamlaka ya China juu ya Kisiwa cha Huangyan cha China.
"Bila idhini ya serikali ya China, ndege ya Ufilipino iliingia kinyume cha sheria kwenye anga ya mamlaka ya China," amesema Tian Junli, msemaji wa eneo hilo la kivita, na ameongeza kuwa upande wa Ufilipino ulieneza maelezo yake ya uwongo.
“Vitendo vya upande wa Ufilipino vimevamia vibaya mamlaka ya China na pia vimevamia vibaya sheria za kimataifa na sheria za China,” Tian amesema.
Kisiwa cha Huangyan ni eneo asili la China, na majaribio ya Ufilipino kudai umiliki haramu wa eneo hilo kupitia uchochezi wa kijeshi na kupotosha uelewa wa kimataifa kwa njia ya fadhaa na kuvumisha mambo hatimaye itakuwa bure, msemaji huyo amesisitiza.
“Vikosi vya eneo la kivita la jeshi la China vinaendelea kuwa katika hali ya tahadhari ili kulinda kithabiti mamlaka na usalama wa nchi na kulinda amani na utulivu katika Bahari ya Kusini,” Tian amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma