Wataalamu wasema China inabaki kuwa nguvu ya kiujenzi katika dunia inayobadilika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 17, 2025

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) akihutubia kwenye kikao cha "China katika Dunia" cha Mkutano wa Usalama wa Munich mjini Munich, Ujerumani, Februari 14, 2025. (Xinhua/Zhang Fan)

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) akihutubia kwenye kikao cha "China katika Dunia" cha Mkutano wa Usalama wa Munich mjini Munich, Ujerumani, Februari 14, 2025. (Xinhua/Zhang Fan)

MUNICH, Ujerumani - Mkutano wa 61 wa Usalama wa Munich (MSC) umehitimishwa mjini Munich, Ujerumani jana Jumapili. Katika mahojiano na Shirika la Habari la China, Xinhua, wataalam wa China waliohudhuria mkutano huo wamesema mkutano huo umeshughulikia hali nyingi zisizo na uhakika zinazoibuka duniani, huku China ikisisitiza dhamira yake ya kuwa nguvu ya kiujenzi katika dunia inayobadilika.

Ripoti ya usalama ilitolewa kabla ya mkutano huo kwa kujikita katika dunia yenye ncha nyingi na sehemu yake ya Marekani imebainisha kuwa serikali ya Marekani chini ya utawala wa Rais Donald Trump "inaahidi ushirikiano wa kimataifa ulio wa chaguo nyingi zaidi, na mara nyingi wenye maamuzi ya upande mmoja, wakati tu maslahi finyu ya Marekani yanapokuwa yanahusika."

Na pia imesema kuwa serikali ya Marekani "kucheza na wazo la kuichukua kwa mabavu Greenland, Panama, na Canada" inaonyesha kuwa haitazuiliwa na kanuni muhimu za kimataifa.

Wang Junsheng, mtafiti katika Taasisi ya Asia-Pasifiki na Mkakati wa Kimataifa ya Akademia ya Sayansi ya Jamii ya China, amesema lengo kuu la mkutano huo lilikuwa ni hali ya kutokuwa na uhakika inayotokana na serikali ya Trump.

Amesema kauli na vitendo vilivyopita vya serikali yake vimeonyesha kutoheshimu utaratibu wa kimataifa na kuvuruga mfumo uliopo wa kimataifa.

Polisi wakilinda karibu na hoteli kunakofanyika Mkuano wa 61 wa Usalama la Munich mjini Munich, Ujerumani, Februari 16, 2025. (Xinhua/Zhang Fan)

Ripoti hiyo imesema serikali ya Trump kutojali mashirika ya Umoja wa Mataifa na mabadiliko ya tabianchi kutaathiri vibaya Nchi za Kusini.

Wang Yiwei, mkurugenzi wa Taasisi ya Masuala ya Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Renmin cha China, amesema kujiondoa kwa Marekani kwenye Mkataba wa Paris na Shirika la Afya Duniani si tu kwamba kunadhoofisha mamlaka na ufanisi wa mfumo wa usimamizi wa dunia lakini pia kumepunguza kasi ya ushirikiano wa pande nyingi.

Kwenye hotuba yake katika MSC, Makamu Rais wa Marekani J.D. Vance amezikosoa nchi za Ulaya, ikiwa ni pamoja na Ujerumani, kuhusu masuala yanayohusu demokrasia na uhamiaji.

Chansela wa Ujerumani Olaf Scholz Jumamosi alimkosoa Vance kwa kuingilia siasa za Ujerumani. Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Noel Barrot siku ya Jumamosi alisisitiza kuwa Ulaya haitakubali kuwekewa mambo kutoka nje.

Xiao Qian, naibu mkuu wa Kituo cha Usalama na Mkakati wa Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Tsinghua cha China, amesema hotuba hiyo ya Vance imeshindwa kushughulikia masuala kama vile mgogoro kati ya Russia na Ukraine na mambo ya ushuru, na kupuuza wasiwasi wa nchi za Ulaya na kwingineko. Maafisa na wasomi wa Ulaya wameelezea kusikitishwa sana.

Polisi wakilinda karibu na hoteli kunakofanyika Mkuano wa 61 wa Usalama la Munich mjini Munich, Ujerumani, Februari 16, 2025. (Xinhua/Gao Jing)

Akihutubia kikao cha "China katika Dunia" cha MSC, Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi ameahidi kwamba China itaendelea kuwa nguvu ya kuleta utulivu duniani na nguvu ya kiujenzi katika dunia inayobadilika.

Wang, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ametoa ufafanuzi kuhusu mitazamo minne muhimu ya China kuhusu kuwepo kwa dunia yenye ncha nyingi, ikiwa ni pamoja na kutetea usawa miongoni mwa mataifa, kuheshimu kanuni ya sheria ya kimataifa, kutekeleza ushirikiano wa pande nyingi, na kushikilia uwazi na ushirikiano wa kunufaishana.

Wataalamu hao wa China wamesema hotuba hiyo ya Wang imeshughulikia wasiwasi wa pande zote na kutoa uhakika mkubwa zaidi katika dunia yenye hali isiyokuwa na uhakika.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha