Ikulu ya Kremlin yasema Putin na Trump watakutana katika nchi ya tatu

(CRI Online) Februari 14, 2025

Msemaji wa Ikulu ya Kremlin ya Russia Dmitry Peskov Alhamisi alipohojiwa na vyombo vya habari alisema, Rais Vladimir Putin wa Russia na mwenzake wa Marekani Donald Trump wamekubali kufanya mkutano wa kikazi katika nchi ya tatu.

Hata hivyo Peskov amesema sehemu ya kufanyia mkutano huo bado haijaamuliwa, akisisitiza kuwa mkutano huo utafanyika kabla ya wakuu wa nchi hizo mbili kutembeleana. Ameongeza kuwa mawasiliano ya kikundi kazi kati ya Russia na Marekani yanatarajiwa kuanzishwa katika siku chache zijazo, ili kufanya maandalizi ya mkutano huo.

Juu ya mazungumzo ya amani yanayoweza kufanyika, msemaji huyo amesema Ukraine itashiriki kwa namna fulani.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha