

Lugha Nyingine
China yapenda kushirikiana na Uingereza ili kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili
Waziri wa Mambo ya Nje wa China ambaye yuko ziarani nchini Uingereza Wang Yi amesema China inapenda kushirikiana na Uingereza ili kuleta msukumu kwa utulivu na kuboresha uhusiano baina ya nchi hizo mbili.
Wang, alisema hayo wakati alipokutana na Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer, ambapo kwanza alimpa salamu za dhati kutoka kwa Rais Xi Jinping, akisema kuwa mkutano uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana kati ya Xi na Starmer umeanzisha mchakato wa kuboresha na kuendeleza uhusiano kati ya China na Uingereza.
Alifafanua kuwa chini ya mwongozo wa kimkakati wa viongozi wa nchi hizo mbili, Mazungumzo ya hivi karibuni ya Kiuchumi na Kifedha kati ya China na Uingereza yanayozaa matunda na mawasiliano katika ngazi zote yamerejeshwa.
Kwa upande wake Starmer alimtaka Wang kuwasilisha salamu zake za dhati kwa Xi, akisema kuwa ushirikiano uliopo kati ya Uingereza na China katika sekta mbalimbali umepata maendeleo mazuri. Ameongeza kuwa anatarajia mazungumzo ya wazi na ya kiujenzi yafanyike kati ya nchi hizo mbili ili kukuza maendeleo endelevu na thabiti ya uhusiano kati ya Uingereza na China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma