Balozi wa China asema vita vya ushuru wa forodha vya Marekani haviwezi kuzuia maendeleo ya China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 14, 2025

Balozi wa China nchini Marekani Xie Feng akishiriki na kutoa hotuba kwenye shughuli za maadhimisho ya miaka 20 ya Shirikisho Kuu la Biashara la China nchini Marekani huko New York, tarehe 11, Februari, 2025. (Xinhua/Li Rui)

Balozi wa China nchini Marekani Xie Feng tarehe 13 alisema, vita vya ushuru wa forodha na vita vya biashara haviwezi kutatua matatizo juu ya uhusiano wa China na Marekani, na pia haviwezi kuzuia maendeleo ya China.

Xie alisema hayo alipotoa hotuba kwenye tamasha la usiku la maadhimisho ya miaka 20 ya Shirikisho Kuu la Biashara la China nchini Marekani lililofanyika Jumanne huko New York, Marekani.

Xie alisema, Marekani kuongeza ushuru wa forodha kwa China kwa kisingizio cha suala la fentanyl “kutaweza kuipelekea kazi iende kinyume chake tu.”

"Tishio la ushuru wa forodha halitafanya kazi kimsingi kwa watu wa China, badala yake litaharibu msingi wa ushirikiano wa China na Marekani katika kupambana na dawa za kulevya na kufanya ushirikiano katika sekta za uchumi na biashara, kuongeza gharama ya familia na kampuni za Marekani, na hatimaye hakutakuwa na mshindi yeyote,” alisema Xie.

Alisema, China inatilia maanani kusukuma mbele maendeleo ya ujenzi wa mambo ya kisasa ya nchini, na Marekani inapendelea zaidi maendeleo ya uchumi wa nchi yake tu . Nchi hizo mbili zinatakiwa kusaidiana na kupata ustawi kwa pamoja badala ya kuzuiana.

Balozi wa China nchini Marekani Xie Feng tarehe 13 alisema, vita vya ushuru wa forodha na vita vya biashara haviwezi kutatua matatizo juu ya uhusiano wa China na Marekani, na pia haviwezi kuzuia maendeleo ya China.

Xie alisema hayo alipotoa hotuba kwenye tamasha la usiku la maadhimisho ya miaka 20 ya Shirikisho Kuu la Biashara la China nchini Marekani lililofanyika Jumanne huko New York, Marekani.

Xie alisema, Marekani kuongeza ushuru wa forodha kwa China kwa kisingizio cha suala la fentanyl "kutaweza kuipelekea kazi iende kinyume chake tu.”

"Tishio la ushuru wa forodha halitafanya kazi kimsingi kwa watu wa China, badala yake litaharibu msingi wa ushirikiano wa China na Marekani katika kupambana na dawa za kulevya na kufanya ushirikiano katika sekta za uchumi na biashara, kuongeza gharama ya familia na kampuni za Marekani, na hatimaye hakutakuwa na mshindi yeyote,” alisema Xie.

Alisema, China inatilia maanani kusukuma mbele maendeleo ya ujenzi wa mambo ya kisasa ya nchini, na Marekani inapendelea zaidi maendeleo ya uchumi wa nchi yake tu. Nchi hizo mbili zinatakiwa kusaidiana na kupata ustawi kwa pamoja badala ya kuzuiana.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha