“Ne Zha 2” yawa filamu ya kwanza ya China inayoweka rekodi mpya ya mauzo ya tiketi ya Yuan Bilioni 10

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 14, 2025

Picha iliyopigwa tarehe 13, Februari, 2025 ikionesha bango la matangazo ya filamu ya katuni ya China “Ne Zha 2” kwenye sinema mjini Beijing, China. (Xinhua/ Ju Huanzong)

Picha iliyopigwa tarehe 13, Februari, 2025 ikionesha bango la matangazo ya filamu ya katuni ya China “Ne Zha 2” kwenye sinema mjini Beijing, China. (Xinhua/ Ju Huanzong)

Takwimu zilizotolewa na tovuti ya Maoyan zinaonesha kuwa, mauzo ya tiketi za filamu ya katuni ya China “Ne Zha 2” sehemu mbalimbali duniani (ambayo ni pamoja na zilizoagizwa) yamezidi Yuan bilioni 10 hadi usiku wa Alhamisi, hali ambayo imefanya filamu hiyo kuwa filamu ya kwanza ya China yenye mauzo ya tiketi ya zaidi ya Yuan 10 (sawa na Dola za Marekani bilioni 1.39).

Filamu hii imeweka rekodi hiyo katika siku ya 16 tangu ianze kuoneshwa kwenye sinema tarehe 29, Januari.

Hapo kabla, “Ne Zha 2” imekuwa filamu ya kwanza ambayo mauzo ya tiketi zake yamefikia Dola za Marekani bilioni 1 katika soko moja, ikiwa ni filamu ya kwanza ya “klabu ya Dola bilioni 1” isiyo ya Hollywood. Vyombo vya kufuatilia mauzo ya tiketi vya Beacon na Maoyan vimekadiri kuwa, mauzo ya jumla ya tiketi za filamu hiyo nchini China hatimaye yatafikia Yuan bilioni 1.5 hadi 1.6.

Wachambuzi walipohojiwa na shirika la habari la China Xinhua Alhamisi walisema, wanaona mafanikio ya “Ne Zha 2” siyo tu yanahusu mauzo ya tiketi yanayoshangaza, bali pia yanahusu filamu hiyo yameonesha vilivyo uhai, mvuto na nguvu halisi ya utamaduni na uvumbuzi wa China.

Wamesema, filamu hiyo iliyopigwa chini ya mwongozaji Yang Yu, aliyejulikana kwa jina la msanii “Jiaozi”, imeweka mnara mpya wa ushawishi wa filamu na utamaduni wa China katika jukwaa la duniani.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha