

Lugha Nyingine
Roboti Shikizi za Mwili kwa Nje zawezesha upandaji milima na kusaidia wazee
Picha iliyopigwa Januari 2025 ikionesha mfanyakazi akijaribu roboti kishikizi za mwili kwa nje kwenye Mlima Tai mkoani Shandong, Mashariki mwa China. (Xinhua)
Wakati wa likizo ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China mwaka huu, Mlima Tai uliopo Mkoa wa Shandong, China ulikuwa moja kati ya vivutio vya watalii vilivyopendwa zaidi na watu, na mlima huo ulianzisha matumizi roboti bunifu shikizi za mwili kwa nje.
Kifaa hicho cha kuvalika, kilichobuniwa kusaidia upandaji wa milima, kimepata ufuatiliaji mkubwa wa watu kwa uwezo wake wa kufanya upandaji Mlima Tai uwe rahisi na kufurahisha zaidi, hasa kwa wazee na watalii wenye changamoto ya kutembea.
“Kweli kinafanya kazi. Mara nilipokivaa, miguu yangu haikuuma tena. Nilihisi kama kuna mtu alikuwa akinivuta juu mlimani,” Li Chengde, mtalii mwenye umri wa miaka 68, amesema baada ya kujaribu kifaa hicho.
Kikiwa kimezalishwa kwa pamoja na Kundi la Kampuni za Utalii wa Utamaduni la Taishan (TCTG) na Kampuni ya Teknolojia ya Kenqing yenye makao yake mjini Shenzhen, roboti hiyo shikizi ya mwili kwa nje, ikiwa na uzito wa kilogramu 1.8 tu, hufungwa kuzunguka kiuno na mapaja ya mvaaji. Ikiwa inaendeshwa na AI, inahisi kasi na mjongeo wa mvaaji, ikitoa usaidizi wa mara moja kupunguza uchovu na maumivu ya viungo.
Kikiwa kilianza kufanya kazi Januari 29 mwaka huu huku vifaa 10 vikiwa vimekodishwa kwa uendeshaji wa majaribio, kifaa hicho kimevutia watumiaji zaidi ya 200 kwa bei ya Yuan 60 (dola za kimarekani 8.37 hivi) hadi 80 kwa kila utumiaji wa mara moja katika eneo hilo la kivutio cha watalii wakati wa likizo hiyo, ambayo ilifikia tamati Februari 4. Nusu ya watu hao waliokodisha roboti hiyo ni wazee.
Wang Houzhe, naibu mkuu wa kamati ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ya TCTG amesema roboti hizo shikizi za mwili kwa nje zimeanzishwa kutoa huduma ili kuwezesha watalii wazee kuwa na fursa ya kujionea uzuri wa mlima huo ana kwa ana.
“Baadhi ya watalii wazee wanataka kufurahia mandhari kando ya njia, lakini kukaa ndani ya kigari cha kebo huzuia uonaji wao. Kupitia usaidizi wa roboti hizi, wanaweza kiukweli kujionea furaha ya kupanda milima,” amesema.
Picha ikionesha roboti shikizi ya mwili kwa nje iliyobuniwa kusaidia upandaji mlima. (Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma