

Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping atuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha rais mwasisi wa Namibia
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ametuma salamu za rambirambi kwa mwenzake wa Namibia, Nangolo Mbumba, kufuatia kifo cha rais mwasisi wa nchi hiyo Sam Nujoma.
Katika salamu hizo zilizotumwa jana Jumatatu, Rais Xi akiwa kwa niaba ya serikali ya China na wananchi wa China, ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Nujoma na kutoa pole kwa familia ya Nujoma, serikali ya Namibia na watu wake.
Rais Xi amesema kuwa Nujoma alikuwa mwanasiasa aliyeheshimiwa sana na ni mwanamapinduzi mzee barani Afrika ambaye alitoa mchango wa kihistoria katika kuongoza watu wa Namibia kwenye harakati za kutafuta uhuru na ukombozi wa taifa hilo, na kupata njia ya maendeleo iliyofaa hali ya nchi hiyo.
“Wakati wote wa maisha yake, aliendelea kuwa rafiki thabiti wa China na kufanya juhudi zaidi za kuhimiza urafiki wa jadi kati ya China na Namibia na ushirikiano kati ya China na Afrika,” Rais Xi amesema.
Rais Xi amesema kuwa kifo cha Nujoma ni hasara kubwa kwa watu wa Namibia, na watu wa China pia wamempoteza rafiki mpendwa wa tangu zamani.
Rais Xi amesema, “Serikali ya China na watu wa China wanathamini sana urafiki wa jadi kati ya China na Namibia,” akieleza imani kwamba kwa juhudi za pamoja za pande zote mbili, uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kati ya China na Namibia hakika utapata maendeleo makubwa zaidi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma