Mpango wa Kimataifa wa Kuvutia "Washirika wa Mji" wa Guangzhou, China wazinduliwa rasmi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 10, 2025

Mpango wa Jumla kwa Kazi Maalum ya “Washirika wa Mji” wa Guangzhou (wa majaribio) umezinduliwa rasmi na kuanza kufanya kazi. Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanywa na Ofisi ya Habari ya Serikali ya Manispaa ya Guangzhou Ijumaa, Februari 8, imeelezwa kwamba kupitia mpango huo wa "Washirika wa Mji", Guangzhou itavutia washirika wa kimkakati, washirika wakubwa, wenye ndoto ya mji huo, na mabalozi wa kuutangaza mji huo kutoka kote duniani, na kuanzisha kwa upana kampeni ya kutafuta watu ambao watafanya kazi pamoja na mji wa Guangzhou ndani na nje ya nchi ili kuiunga mkono, kuwekeza na kuiendeleza Guangzhou pamoja.

Zhu Xiaoyi, Naibu Katibu Mkuu wa Serikali ya Manispaa ya Guangzhou, amesema kuwa Mpango huo wa "Washirika wa Mji" wa Guangzhou unajikita katika maeneo muhimu ya ujenzi wa chapa na uendelezaji wa tasnia za mji, kuvutia pamoja mjini humo makundi ya kampuni, taasisi na watu binafsi ambao wanaweza kutoa rasilimali mbalimbali kwa ajili ya maendeleo bora ya hali ya juu ya Guangzhou, kama "Washirika wa Mji" wa Guangzhou.

Mkutano na waandishi wa habari ukifanyika. (Picha kutoka CNR)

Mkutano na waandishi wa habari ukifanyika. (Picha kutoka CNR)

Ni kwa namna gani Mpango wa “Washirika wa Mji”jumlisha“Michezo ya Taifa ya China”vitapata matokeo ya “1+1>2”?

“Tutajenga juu ya jukwaa la ujenzi wa pamoja wa mpango wa 'washirika wa mji', na kutumia fursa ya 'Mwaka wa Michezo ya Kitaifa' wa 2025 ili kutumia kikamilifu faida za Guangzhou kama mwenyeji wa hafla ya ufunguzi na eneo kuu la mashindano. Tutatumia shughuli za michezo hiyo kukuza faida za mji, kufungamanisha kwa kina rasilimali za michezo na rasilimali za mji, kufungamanisha kwa ufanisi rasilimali mbalimbali za mji, na kuwezesha‘washirika wa mji’kutoka nje ya mzunguko wao." Zhu Xiaoyi ameongeza.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha