

Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping atoa wito wa kuhimiza ustawishaji kamili wa eneo la kaskazini mashariki mwa China
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitoa hotuba muhimu baada ya kusikiliza ripoti ya kazi kutoka kwa Kamati ya Chama ya Mkoa wa Jilin na serikali ya mkoa huo huko Changchun, Mkoa wa Jilin, kaskazini mashariki mwa China, Februari 8, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)
CHANGCHUN - Rais wa China Xi Jinping amehimiza Mkoa wa Jilin kutekeleza zaidi mipango ya kimkakati ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kuhusu kustawisha kwa pande zote eneo la kaskazini mashariki mwa China katika zama mpya na kutekeleza kithabiti jukumu kubwa zaidi katika kuendeleza ujenzi wa mambo ya kisasa wa China.
Rais Xi ametoa maagizo hayo baada ya kusikiliza ripoti ya kazi ya Kamati ya chama ya mkoa wa Jilin na serikali ya mkoa huo huko Changchun, mji mkuu wa mkoa wa Jilin siku ya Jumamosi.
Rais Xi akisisitiza kwamba mkoa wa Jilin lazima ujikite kwenye msingi wa kujipatia maendeleo ya sifa bora, kuendeleza bila kuyumbayumba uchumi halisi ambao ni msingi wa mkoa huo, na kufanya mpango wa jumla wa kuvifanyia mageuzi viwanda vya jadi, kuimarisha viwanda vyenye nguvu ya ushindani, na kujenga nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora.
“Juhudi pia zinapaswa kufanywa ili kuyafanya mafanikio ya kiteknolojia kuwa tija halisi,” amesema.
Amesema kuwa kuendeleza kwa kina mageuzi na ufunguji mlango ni muhimu zaidi kwa ustawishaji wa pande zote wa eneo la kaskazini mashariki mwa China.
“Sera na sheria na kanuni husika lazima zitekelezwe kikamilifu katika mchakato wa kuendeleza kwa kina mageuzi ya viwanda vya kiserikali na kuhimiza maendeleo ya uchumi wa kibinafsi,” Rais Xi amesema.
Amesisitiza umuhimu wa kujenga mazingira ya biashara ya maendeleo ya kiwango cha juu yaliyo kwenye soko, usimamizi wa kisheria na kimataifa, na kujenga mfumo mpya wa uchumi wa kufungua mlango wa kiwango cha juu zaidi.
Amehimiza mkoa wa Jilin kuweka kipaumbele cha juu katika maendeleo ya kilimo cha kisasa na kikubwa, kufanya mpango wa jumla wa kuendeleza kilimo cha kiteknolojia, kilimo cha kijani, kilimo cha sifa bora na kilimo cha chapa maarufu.
Eneo la Kaskazini Mashariki mwa China linajumuisha mikoa ya Heilongjiang, Jilin na Liaoning, kwa muda mrefu limekuwa vituo muhimu vya viwanda na kilimo, haswa katika kipindi cha mwanzo baada ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China. Kustawisha eneo hilo la kaskazini mashariki mwa China ni mkakati mkubwa wa Kamati Kuu ya CPC kwa ajili ya maendeleo ya jumla ya nchi ya China.
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitoa hotuba muhimu baada ya kusikiliza ripoti ya kazi ya Kamati ya Chama ya mkoa wa Jilin na Serikali ya mkoa huo huko Changchun, Mji Mkuu wa Jilin, kaskazini mashariki mwa China, Februari 8, 2025. (Xinhua/Yan Yan)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma