

Lugha Nyingine
Michezo ya 9 ya Majira ya Baridi ya Asia yafunguliwa mjini Harbin, China
(Xinhua/Wang Ye)
HARBIN - Rais wa China Xi Jinping amefungua Michezo ya 9 ya Majira ya Baridi ya Asia mjini Harbin jana Ijumaa usiku kwenye hafla ya shamrashamra nyingi ikionyesha utamaduni wa barafu na theluji wa mji huo ambapo zaidi ya watazamaji 8,000 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano, Maonyesho na Michezo wa Harbin walitoa vifijo na vigelegele vya furaha wakati Rais Xi akitangaza rasmi michezo hiyo kufunguliwa mbele ya viongozi wakuu walioko ziarani China akiwemo Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki Thomas (IOC)
Ufunguzi wa michezo hiyo ulifikia kilele chake ambapo wabeba mwenge wanne - bingwa mara mbili wa Olimpiki na mwanariadha wa mbio fupi za kuteleza kwenye theluji Yang Yang, mshindi wa medali ya dhahabu ya Olimpiki ya Majira ya Baridi wa kwanza wa China kwa wanamume na mwanamichezo wa kuteleza kwenye theluji kwa mtindo huru Han Xiaopeng, bingwa wa mbio za kutembea kwa haraka za Olimpiki Wang Zhen, na bingwa wa mchezo wa kuteleza kwa kasi kwenye theluji wa Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Sochi Zhang Hong - waliambatana na watoto walioshika taa za kijadi za barafu, wakiangaza uwanja wenye umbo la lilac kwenye ukumbi mdogo wa ufunguzi wa michezo, Bustani ya Theluji na Barafu ya Harbin, ambayo ni bustani kubwa zaidi ya mandhari ya barafu na theluji duniani.
Ikiwa imepangwa kufanyika kuanzia Februari 7 hadi 14, Michezo hiyo ya Harbin, yenye kauli mbiu "Ndoto ya Pamoja ya Majira ya Baridi, Moyo Mmoja wa Asia" ni michezo mingine mkubwa ya kimataifa ya majira ya baridi iliyoandaliwa na China kufuatia Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing mwaka 2022. Pia ni mara ya tatu kwa nchi ya China kuandaa Michezo ya Majira ya Baridi ya Asia, kufuatia Harbin 1996 na Changchun 2007.
Rekodi ya nchi na maeneo washiriki 34 katika Michezo ya Harbin 2025, ikipita rekodi ya juu iliyowekwa awali katika Michezo ya 8 ya Majira ya Baridi ya Asia mjini Sapporo, Japan mwaka 2017.
Zaidi ya wanamichezo 1,200 wanashiriki katika mashindano ya michezo kwenye theluji huko Harbin na mashindao ya michezo kwenye theluji katika eneo la Yabuli, ikionesha ongezeko kutoka rekodi ya awali ya 1,147 katika Michezo ya Sapporo.
Ujumbe wa China umeundwa na watu 257, wakiwemo wanamichezo 170. Mabingwa watano wa Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022, Xu Mengtao, Qi Guangpu, Gao Tingyu, Fan Kexin na Liu Shaoang wanaongoza wanamichezo wa kiume 85 na wanamichezo wa kike 85 ambao watashiriki kwenye mashindano ya michezo 64 ya aina sita.
Rais wa China Xi Jinping akishiriki kwenye ufunguzi wa Michezo ya 9 ya Majira ya Baridi ya Asia mjini Harbin, Mkoa wa Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China, Februari 7, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)
Rais wa China Xi Jinping akipunga mkono kwenye ufunguzi wa Michezo ya 9 ya Majira ya Baridi ya Asia mjini Harbin, Mkoa wa Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China, Februari 7, 2025. (Xinhua/Yan Yan)
Xi Jinping na viongozi wengine wa Chama na serikali wakishiriki kwenye ufunguzi wa Michezo ya 9 ya Majira ya Baridi ya Asia mjini Harbin, Mkoa wa Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China, Februari 7, 2025. (Xinhua/Yan Yan)
Rais wa China Xi Jinping akipunga mkono kwenye ufunguzi wa Michezo ya 9 ya Majira ya Baridi ya Asia mjini Harbin, Mkoa wa Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China, Februari 7, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma