Rais Xi asema China na Korea Kusini zinapaswa kuimarisha uhusiano chini ya kuongezeka kwa hali ya kutokuwa na uhakika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 08, 2025

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Spika wa Bunge la Korea Kusini Woo Won-shik mjini Harbin, Mkoani Heilongjiang, kaskazini-mashariki mwa China, Februari 7, 2025. (Xinhua/Yue Yuewei)

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Spika wa Bunge la Korea Kusini Woo Won-shik mjini Harbin, Mkoani Heilongjiang, kaskazini-mashariki mwa China, Februari 7, 2025. (Xinhua/Yue Yuewei)

HARBIN - Rais Xi Jinping wa China siku ya Ijumaa alipokutana na Spika wa Bunge la Korea Kusini Woo Won-shik mjini Harbin, Mkoani Heilongjiang, China ambaye alikuwa ziarani mjini humo kushiriki ufunguzi wa Michezo ya 9 ya Majira ya baridi ya Asia, amesema China na Korea Kusini zinapaswa kufanya kazi pamoja ili kuimarisha ushirikiano wao wa kiwenzi na kimkakati, chini ya kuongezeka kwa hali ya kikanda na dunia ya kutokuwa na uhakika.

“Tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia zaidi ya miaka 30 iliyopita, nchi hizo mbili zimeendeleza uhusiano wao na kuongeza ushirikiano kati yao, ikitoa mchango kwa ajili ya amani na maendeleo ya kikanda,” Rais Xi amesema, akibainisha kuwa sera ya China kuhusu Korea Kusini inaendelea kuwa thabiti.

Ametoa wito kwa nchi hizo mbili kuzidisha uhusiano wao wa kunufaishana wa kiuchumi na kibiashara na kuongeza mawasiliano ya kitamaduni na ya kati ya watu na watu.

Kwa upande wake Woo amesema kudumisha uhusiano wa kirafiki na China ni sera kuu ya mambo ya nje ya Korea Kusini.

“Korea Kusini inapenda kushirikiana na China ili kuinua uhusiano kati ya pande mbili hadi ngazi mpya katika mwaka mpya,” Woo ameongeza, huku pia akieleza matumaini kuwa nchi hizo mbili zitaimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara, kuhakikisha utulivu wa minyororo ya kimataifa ya viwanda na usambazaji, na kupanua mawasiliano kati ya watu.

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Spika wa Bunge la Korea Kusini (ROK) Woo Won-shik mjini Harbin, Mkoani Heilongjiang, kaskazini-mashariki mwa China, Februari 7, 2025. (Xinhua/Ding Haitao)

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Spika wa Bunge la Korea Kusini (ROK) Woo Won-shik mjini Harbin, Mkoani Heilongjiang, kaskazini-mashariki mwa China, Februari 7, 2025. (Xinhua/Ding Haitao)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha