Rais Xi Jinping wa China akutana na Waziri Mkuu wa Thailand Paetongtarn Shinawatra mjini Beijing

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 07, 2025

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri Mkuu wa Thailand Paetongtarn Shinawatra, ambaye yuko ziarani nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Februari 6, 2025. (Xinhua/Liu Weibing)

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri Mkuu wa Thailand Paetongtarn Shinawatra, ambaye yuko ziarani nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Februari 6, 2025. (Xinhua/Liu Weibing)

BEIJING - Rais Xi Jinping wa China amekutana na Waziri Mkuu wa Thailand Paetongtarn Shinawatra mjini Beijing siku ya Alhamisi akisema kwamba mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Thailand na "Jubilee ya Dhahabu ya Urafiki wa China na Thailand."

"Pande hizo mbili zinapaswa kuendelea na mafanikio ya zamani na kufanya kazi pamoja kuendeleza ujenzi wa jumuiya ya China na Thailand yenye mustakabali wa pamoja ili kutoa manufaa zaidi kwa watu wa nchi hizo mbili, na kunufaisha zaidi kanda hiyo na dunia kwa ujumla," Rais Xi amesema.

Amesema, katika kukabiliana na mabadiliko makubwa ambayo hayajaonekana katika miaka 100 iliyopita, China na Thailand zinapaswa kuimarisha hali ya kuaminiana kimkakati, kuungana mkono kithabiti, na kuitikia hali ya kutokuwa na uhakika katika mazingira ya nje kwa utulivu na uhakika wa uhusiano kati ya China na Thailand.

"China inapenda kushirikiana na Thailand kuunganisha mikakati ya maendeleo, kupanua ushirikiano wa kunufaishana, kutekeleza vyema miradi kinara kama vile Reli ya China na Thailand, na kuhimiza dira ya maendeleo yaliyounganishwa ya China, Laos na Thailand ili kupata matokeo yenye manufaa zaidi mapema iwezekanavyo," amesema.

Rais Xi ametoa wito wa kufanya juhudi za pamoja ili kuzidisha ushirikiano katika sekta zinazoibukia kama vile uchumi wa kidijitali na magari yanayotumia nishati mpya, na kujenga minyororo ya viwanda na usambazaji iliyo imara na tulivu zaidi.

Akibainisha kuwa China inathamini hatua madhubuti za Thailand dhidi ya kamari na ulaghai wa mtandaoni, Rais Xi amesema pande zote mbili zinapaswa kuendelea kuimarisha usimamizi wa utekelezaji wa sheria, ushirikiano wa usalama na kisheria ili kulinda usalama wa maisha na mali za watu vilevile mawasiliano yenye utaratibu na ushirikiano kati ya nchi za kikanda.

"China inapenda kushirikiana kwa karibu na Thailand ili kutetea kithabiti mfumo wa kimataifa huku Umoja wa Mataifa ukiwa katika msingi wake na utaratibu wa kimataifa unaotilia maanani sheria ya kimataifa, kuimarisha umoja na ushirikiano katika Nchi za Kusini, kulinda amani ya dunia na kuhimiza maendeleo ya pamoja," amesema.

Kwa upande wake Paetongtarn amesema amefurahi kutembelea China wakati ambapo nchi hizo mbili zinasherehekea "Jubilee ya dhahabu" ya urafiki wao. Amesema, Thailand na China zimeunda uhusiano maalum wa kirafiki na kiwenzi katika miongo mitano iliyopita.

Akisisitiza tena Thailand kushikilia sera ya kuwepo kwa China moja, amesema Thailand inatarajia kushirikiana na China ili kuongeza mawasiliano ya ngazi ya juu, kuimarisha ushirikiano katika nyanja za mawasiliano, uchumi, biashara na kilimo, na kuhimiza mawasiliano kati ya watu na watu ili kuingia katika miongo mitano ijayo ya kunufaisha pamoja amani na ustawi.

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri Mkuu wa Thailand Paetongtarn Shinawatra, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Februari 6, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri Mkuu wa Thailand Paetongtarn Shinawatra, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Februari 6, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha