

Lugha Nyingine
Rais Xi kuhudhuria hafla ya ufunguzi wa Michezo ya 9 ya Majira ya Baridi ya Asia
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping atahudhuria hafla ya ufunguzi wa Michezo ya 9 ya Majira ya Baridi ya Asia, ambayo itafanyika leo Ijumaa mjini Harbin, Mkoa wa Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China.
Kiongozi huyo atatangaza Michezo hiyo kufunguliwa rasmi.
Rais Xi ataandaa dhifa ya ukaribisho wa viongozi wa kigeni watakaohudhuria hafla hiyo ya ufunguzi, akiwemo Sultani wa Brunei Haji Hassanal Bolkiah Mu'izzaddin Waddaulah, Rais wa Kyrgyzstan Sadyr Japarov, Rais wa Pakistan Asif Ali Zardari, Waziri Mkuu wa Thailand Paetongtarn Shinawatra, na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Korea Woo Won-shik.
Hafla hiyo ya ufunguzi itaonyeshwa moja kwa moja na Shirika Kuu la Utangazaji la China. Tovuti ya Shirika la Habari la China, Xinhuanet itatoa matangazo ya moja kwa moja kwa picha na ripoti.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma