

Lugha Nyingine
Huawei yaanza kutoa mafunzo kwa washindi wa Kenya kwenye mashindano ya TEHAMA
Kampuni ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ya Huawei ya China imeanzisha programu ya mafunzo kwa wanafunzi 18 wa vyuo vikuu vya Kenya waliopata ushindi katika shindano la kitaifa la ujuzi wa kidijitali ili kuwaandaa kwa ajili ya mashindano ya kikanda yatakayofanyika baadaye mwezi huu.
Taarifa iliyotolewa Jumatano na Huawei mjini Nairobi imeeleza kuwa, mafunzo hayo yanafuatilia teknolojia za hali ya juu za habari na mawasiliano, ikiwa ni pamoja na uundaji wa mitandao, cloud computing, na akili mnemba (AI), yakilenga kuwapa wanafunzi hao ujuzi hitajika wa kiutendaji katika mashindano yajayo ya kikanda.
Mkuu wa programu ya mafunzo ya TEHEMA ya Huawei nchini Kenya Bw. Michael Kamau, amesisitiza dhamira ya kampuni hiyo ya kuboresha ujuzi wa kidijitali kwa vijana wa nchi hiyo ili kuchochea ukuaji wa uchumi, kuongeza nafasi za ajira na kuhimiza maendeleo ya kijamii.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma