Rais Xi Jinping afanya mazungumzo na Rais wa Pakistan Asif Ali Zardari

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 06, 2025

Rais Xi Jinping wa China akipeana mkono na Rais Asif Ali Zardari wa Pakistan kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Februari 5, 2025. (Xinhua/Li Xueren)

Rais Xi Jinping wa China akipeana mkono na Rais Asif Ali Zardari wa Pakistan kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Februari 5, 2025. (Xinhua/Li Xueren)

BEIJING - Rais Xi Jinping wa China amefanya mazungumzo na Rais Asif Ali Zardari wa Pakistan mjini Beijing siku ya Jumatano akisema kuwa China na Pakistan zina urafiki imara na ni washirika wa ushirikiano wa kimkakati kwa siku zote.

Amesema, katika miaka ya hivi karibuni, nchi hizo mbili zimeshikilia kuungana mkono katika mambo ya siasa, kudumisha mawasiliano ya karibu ya ngazi ya juu, na kuendeleza ujenzi wa Ukanda wa Kiuchumi wa China na Pakistan na ushirikiano katika nyanja mbalimbali, ukiweka mfano mzuri kwa uhusiano kati ya nchi na nchi.

“China inapenda kushirikiana na Pakistan ili kuendeleza jitihada zao husika za ujenzi wa mambo ya kisasa, kuharakisha ujenzi wa jumuiya iliyo karibu zaidi kati ya China na Pakistan yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya, kuleta manufaa zaidi kwa watu wa nchi hizo mbili, na kutoa mchango mkubwa zaidi kwa amani, utulivu na ustawi wa kikanda,” Rais Xi amesema.

Rais Xi amesisitiza kuwa China daima inatazama uhusiano wake na Pakistan kwa muono wa kimkakati, na inadumisha kiwango cha juu cha utulivu na uendelevu katika sera yake ya kirafiki kuhusu Pakistan. Amesema China, kama inavyofanya wakati wote, itaiunga mkono Pakistan kwa uthabiti katika kulinda mamlaka, uhuru na ukamilifu wa ardhi yake, katika kupambana na ugaidi, na kufuata njia ya maendeleo inayoendana na hali yake halisi ya kitaifa.

Ametoa wito kwa nchi hizo mbili kuyafanya mikakati ya maendeleo yaendane zaidi na kuzidisha mawasiliano ya uzoefu wa utawala, kuimarisha mawasiliano katika ngazi zote na katika mamlaka zote, na kuimarisha msingi wa kisiasa wa uhusiano kati ya China na Pakistan.

Pakistan itasimama kidete na China bila kujali jinsi hali itabadilika, Rais Zardari amesema, huku akielezea shukrani za Pakistan kwa msaada ambao China imekuwa ikitoa kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Pakistan.

Amesema Pakistan inapenda kujifunza uzoefu wa China wenye mafanikio na kuhimiza maendeleo bora ya hali ya juu ya Ukanda wa Kiuchumi wa China na Pakistan na ushirikiano katika nyanja mbalimbali, ili kufikia maendeleo ya viwanda na ujenzi wa mambo ya kisasa.

Amesema, chini ya uongozi wa Rais Xi, China imekuwa na jukumu muhimu la kiuongozi katika masuala ya kimataifa na imekuwa nguvu muhimu zaidi kwa ajili ya amani, utulivu na ustawi wa dunia.

Baada ya mazungumzo yao, wakuu hao wa nchi walishuhudia utiaji saini nyaraka kadhaa za ushirikiano wa pande mbili kuhusu Ukanda wa Kiuchumi wa China na Pakistan, biashara, sayansi na teknolojia, na redio na televisheni.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha