Xi Jinping atoa salamu za Mwaka Mpya wa Jadi wa China kwa watu wasio wanachama wa CPC

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 21, 2025

Xi Jinping, Rais wa China, ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) na Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ameshiriki kwenye mkusanyiko wa mwaka na watu wasio wanachama wa CPC kabla ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Januari 20, 2025. (Xinhua/Yan Yan)

Xi Jinping, Rais wa China, ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) na Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ameshiriki kwenye mkusanyiko wa mwaka na watu wasio wanachama wa CPC kabla ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Januari 20, 2025. (Xinhua/Yan Yan)

BEIJING - Xi Jinping, Rais wa China, ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) na Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ametoa salamu za sikukuu kwa watu kutoka vyama mbalimbali vya kidemokrasia, na mashirikisho ya wanaviwanda na wafanyabiashara ya China, na watu wasio na vyama, pamoja na watu wengine wa umoja wa mstari wa mbele kabla ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China.

Rais Xi, ametuma salamu hizo jana Jumatatu aliposhiriki kwenye mkusanyiko wa mwaka na watu wasio wanachama wa CPC kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing. Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, kwa kalenda ya kilimo ya China, itaangukia Januari 29 mwaka huu.

Akikumbuka mafanikio ya mwaka 2024, Rais Xi amesema kuwa China imeshinda matatizo na kupiga hatua za kusonga mbele, ikitimiza malengo na majukumu makuu ya mwaka huo ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

"Tumeongoza sekta zote katika ngazi zote kutumia kwa usahihi mazingira yaliyotusaidia na kushughulikia mambo yasiyoweza kutusaidia, kudumisha dhamira ya kimkakati, na kuimarisha imani yetu katika ushindi," amesema.

Rais Xi amesema kuwa China imetekeleza sera mbalimbali kwa ufanisi, imetoa mfululizo wa sera za nyongeza, na kuhimiza kwa hatua madhubuti maendeleo ya sifa bora.

“Uchumi umeonyesha dalili za kuimarika, ukifikia ukuaji wa Pato la Taifa wa asilimia 5,” ameongeza.

Ameeleza kuwa, msururu wa mafanikio mapya yamepatikana katika mstari wa mbele wa sayansi na teknolojia, yakihimiza kwa kiasi kikubwa maendeleo ya nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora.

Amesisitiza kufanya juhudi za kuendeleza zaidi mageuzi kwa kina, kulinda amani na utulivu wa Dunia, kuhimiza maendeleo ya binadamu, na kufanya juhudi za kuboreha mienendo ya kazi ya Chama na serikali.

Rais Xi pia amesisitiza maendeleo ya hali motomoto ya mambo ya ushirikiano wa vyama vingi.

Amesema China itatekeleza sera za jumla za kuhimiza juhudi zaidi na zenye matokeo, kujikita katika maendeleo ya sifa bora na kuhimiza kujitegemea na kuongeza nguvu zaidi katika sayansi na teknolojia ili kudumisha kasi nzuri ya maendeleo ya jamii na uchumi katika mwaka 2025.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha