

Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping atoa salamu za Mwaka Mpya wa Jadi wa China kwa wanajeshi wastaafu
![]() |
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitoa salamu za Mwaka Mpya wa Jadi wa China kwa wanajeshi wastaafu wa nchi hiyo wakati aliposhiriki kwenye tamasha lililoandaliwa na CMC kwa maafisa wastaafu wa kijeshi wa vikosi vya jeshi la eneo la Beijing, Januari 17, 2025. (Xinhua/Li Gang) |
EIJING - Rais wa China Xi Jinping aliposhiriki kwenye tamasha lililoandaliwa na Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) kwa ajili ya maafisa wastaafu wa kijeshi wa vikosi vya jeshi la eneo la Beijing siku ya Ijumaa, ametoa salamu za Mwaka Mpya wa Jadi wa China kwa wanajeshi wote wastaafu wa nchi hiyo.
Rais Xi, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa CMC, aliungana na wanajeshi hao huku wakimpigia makofi ya furaha, akiwauliza juu ya afya na hali zao za maisha. Walikumbuka pamoja safari isiyo ya kawaida ya Chama, nchi na jeshi na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika mwaka uliopita.
Wanajeshi hao wastaafu wameapa kushikamana kwa karibu zaidi na Kamati Kuu ya CPC ambayo Komredi Xi Jinping ni kiongozi wake, kufuata kwa uthabiti mwongozo wa Fikra ya Xi Jinping juu ya Ujamaa wenye Umaalum wa China kwa Zama Mpya, na kutekeleza fikra ya Xi Jinping juu ya kuimarisha jeshi.
Wameahidi kufuata desturi nzuri, kudumisha uadilifu wa kisiasa, na kutoa mchango mpya kwa ajili ya kujenga nchi yenye nguvu kwa pande zote na kufikia ustawishaji wa taifa katika kufuata njia ya ujenzi wa mambo ya kisasa yenye umaalumu wa China.
Sikukuu ya mwaka huu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, kwa kalenda ya kilimo ya China, itaangukia Januari 29.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma