Rais Xi Jinping atoa wito wa kuhimiza mambo muhimu mapya katika ushirikiano wa China na Sri Lanka

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 16, 2025

Rais wa China Xi Jinping akipeana mkono na Rais wa Sri Lanka Anura Kumara Dissanayake kwenye Jumba la Mikutano ya Umma  la Beijing,  China, Januari 15, 2025. (Xinhua/Ding Lin)

Rais wa China Xi Jinping akipeana mkono na Rais wa Sri Lanka Anura Kumara Dissanayake kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Januari 15, 2025. (Xinhua/Ding Lin)

BEIJING – Januari 15, Rais Xi Jinping wa China alikuwa na mazungumzo na Rais wa Sri Lanka Anura Kumara Dissanayake, ambaye yuko ziarani nchini China, ambapo alisema, China itafanya juhudi za kuiunga mkono Sri Lanka katika kujikita kwenye maendeleo ya uchumi, na nchi hizo mbili zinapaswa kuhimiza kwa pamoja mambo muhimu mapya katika ujenzi wa sifa bora wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, vilevile ushirikiano katika kilimo cha kisasa, uchumi wa kidijitali na uchumi wa baharini.

“Jitihada za China katika kuendeleza zaidi mageuzi ya kina ili kuhimiza ujenzi wa mambo ya kisasa wa China zitaleta fursa mpya kwa maendeleo ya Sri Lanka,” Rais Xi amesema.

Xi amedhihrisha kuwa China na Sri Lanka zinafurahia urafiki wa jadi katika miaka 68 iliyopita, uhusiano wa pande mbili umedumisha maendeleo mazuri na thabiti, ukitoa mfano wa kuishi pamoja kwa urafiki na kufanya ushirikiano wa kunufaishana kati ya nchi mbalimbali.

“Kwa juhudi za pamoja, China na Sri Lanka zimeendelea kuhimiza uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati unaosaidiana na kuwa na urafiki wa kudumu,” Rais Xi amesema, akiongeza kuwa, ujenzi wa sifa bora wa Ukanda Mmoja, Njia Moja na ushirikiano katika sekta mbalimbali umepata matokeo yenye matunda, yakileta manufaa halisi kwa watu wa nchi hizo mbili.

"Nchi zetu mbili zinapaswa kuendeleza uhusiano wa pande mbili kutoka kwenye mtazamo wa kimkakati na kujenga kwa pamoja jumuiya ya China na Sri Lanka yenye mustakabali wa pamoja," amesema.

Rais Xi amesema kuwa China inaichukulia Sri Lanka kama kipaumbele cha juu katika mambo ya diplomasia yake ya ujirani, na China itaendelea kuiunga mkono Sri Lanka katika kulinda uhuru, mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi.

Ametoa wito wa kukusanya juhudi za pamoja za Nchi za Kusini, kuhimiza mshikamano na maendeleo, na kutoa mchango kwa ajili ya amani, utulivu na ustawi wa kikanda.

Rais Dissanayake amesema kuwa Sri Lanka inapongeza sana mafanikio makubwa ya maendeleo ya China katika uchumi, sayansi na teknolojia, na miundombinu, China siku zote imekuwa rafiki na mshirika wa kutegemewa wa Sri Lanka, na Sri Lanka inaweka umuhimu mkubwa kwenye uhusiano wake na China.

“Sri Lanka inafuata kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja, na kushukuru uungaji mkono wenye thamani wa China katika kulinda uhuru, mamlaka ya nchi na haki na maslahi halali ya Sri Lanka,” Rais Dissanayake amesema.

Baada ya mazungumzo hayo, marais hao wa nchi kwa pamoja walishuhudia utiaji saini wa nyaraka kadhaa za ushirikiano wa pande mbili katika ujenzi wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, mazao ya kilimo, huduma za jamii, habari na utangazaji.

Rais Xi Jinping wa China akifanya hafla ya kumkaribisha Rais wa Sri Lanka Anura Kumara Dissanayake katika Ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing kabla ya mazungumzo yao Januari 15, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)

Rais Xi Jinping wa China akifanya hafla ya kumkaribisha Rais wa Sri Lanka Anura Kumara Dissanayake katika Ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing kabla ya mazungumzo yao Januari 15, 2025. (Xinhua/Zhang Ling)

Rais Xi Jinping wa China akifanya hafla ya kumkaribisha Rais wa Sri Lanka Anura Kumara Dissanayake katika Ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing kabla ya mazungumzo yao Januari 15, 2025. (Xinhua/Yao Dawei)

Rais Xi Jinping wa China akifanya mazungumzo na Rais wa Sri Lanka Anura Kumara Dissanayake, ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing Januari 15, 2025. (Xinhua/Zhang Ling)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha