Rais Xi asema uhusiano wa washirika wa China na Umoja wa Ulaya ni moja kati ya uhusiano wa washirika wa kunufaishana

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 15, 2025

BEIJING – Alasiri ya Januari 14, Rais Xi Jinping wa China alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na Mwenyekiti wa Baraza la Ulaya Antonio Costa, ambapo akisisitiza kuwa, hakuna mgongano wa maslahi ya kimsingi au migogoro ya siasa za kijiografia kati ya China na Umoja wa Ulaya (EU), pande hizo ni washirika ambao wanaweza kuchangia kwenye mafanikio ya kila mmoja wao.

Kwenye mazungumzo hayo, Rais Xi ametoa pongezi zake kwa mara nyingine tena kwa Costa kwa kuchukua wadhifa wa mwenyekiti wa Baraza la Ulaya, akisema kuwa mwaka huu ni wa maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na EU, ambapo ni wakati muhimu kwa kuendeleza mambo yaliyofanyika huko nyuma.

“Historia ya uhusiano kati ya China na EU inadhihirisha kwamba kama pande zote mbili zinashikilia kuheshimiana, kutendeana kwa usawa, na kufanya mazungumzo ya wazi, zinaweza kuendeleza ushirikiano na kupata mafanikio makubwa” Rais Xi amesema.

Amesema, kuwa na nia moja kunaleta ushirikiano, na kutafuta maelewano ya pamoja huku kukiwa na kuheshimu tofauti pia kunaweza kuleta ushirikiano.

“Jambo la muhimu liko katika kuheshimu chaguo la kila mmoja la mfumo wa jamii na njia ya maendeleo, vilevile maslahi ya kimsingi na masuala yanayofuatiliwa na kila mmoja,” Rais Xi amesema, akiongeza kuwa China siku zote imekuwa ikiichukulia Ulaya kama ncha muhimu katika dunia ya ncha nyingi, ikiunga mkono kithabiti umoja wa Ulaya, na kuunga mkono EU kujiamulia kimkakati.

Rais Xi akitoa wito kwa pande zote mbili kuimarisha mawasiliano ya kimkakati, kuongeza hali ya kuaminiana kimkakati, na kushikilia uhusiano wa washirika kati ya pande mbili, amesema kuwa China inaendelea kuwa na imani na EU na inatumai EU pia itakuwa mshirika wa kuaminika wa ushirikiano kwa China.

Rais Xi amesema kuwa China inaendelea kuwa na dhamira kwa maendeleo ya sifa bora na kupanua ufunguaji mlango wa kiwango cha juu, na hii italeta fursa mpya kwa ushirikiano kati ya China na Umoja wa Ulaya.

Kwa upande wake, Costa amesema kuwa mwaka 2025 ni mwaka muhimu kwa uhusiano wa EU na China, na upande wa EU unapenda kusherehekea pamoja na China miaka 50 ya uhusiano kati yao, kuimarisha mazungumzo na mawasiliano, kuongeza hali ya kuaminiana kimkakati, kuimarisha uhusiabo wa washirika , na kufungua mustakabali mzuri wa uhusiano wa EU na China.

Costa amesema, “ Umoja wa Ulaya unapenda kushughulikia ipasavyo tofauti za kiuchumi na kibiashara na China kwa kupitia mazungumzo na mashauriano,” pande mbili EU na China zinaheshimu nia ya Katiba ya Umoja wa Mataifa, kushikilia ushirikiano wa pande nyingi, kulinda biashara huria, na kupinga makabiliano ya kambi na zinapaswa kufanya ushirikiano badala ya ushindani.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha