Rais Xi Jinping akutana na Waziri Mkuu wa Grenada, atoa wito wa kuendeleza uhusiano wa pande mbili

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 14, 2025

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Waziri Mkuu wa Grenada Dickon Mitchell, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Januari 13, 2025. (Xinhua/Ding Lin)

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping siku ya Jumatatu alipokutana na Waziri Mkuu wa Grenada Dickon Mitchell, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, amesema kuwa China inapenda kutoa msaada kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Grenada ndani ya mfumokazi wa ushirikiano wa Kusini na Kusini.

Amesema, nchi hizo mbili zinapaswa kuanzisha na kuendeleza mambo muhimu mapya ya ushirikiano katika sekta ya nishati mpya, maendeleo ya kijani na yenye kutoa kaboni chache, na uchumi wa kidijitali.

Mitchell kwanza alitoa salamu za dhati za pole na rambirambi kwa serikali ya China na watu wake kutokana na tetemeko kubwa la ardhi lililotokea hivi karibuni katika Wilaya ya Dingri ya Mkoa unaojiendesha wa Xizang, kusini-magharibi mwa China.

Rais Xi ameelezea shukrani zake kwa hilo. Huku akieleza kuwa tetemeko hilo la ardhi lilitokea katika eneo la mwinuko wa juu kutoka usawa wa bahari, China imekamilisha kazi ya uokoaji na kuwahamisha watu waliokumbwa na tetemeko hilo kwenye makazi ya muda katika muda mfupi kwa iwezekanavyo na itafanya kazi ya ukarabati mpya baada ya maafa haraka iwezekanavyo.

"Serikali ya China ina imani na uwezo wa kupata mafanikio katika kukabiliana na tetemeko la ardhi," Rais Xi amesema.

Rais Xi amsema kuwa katika miaka ya hivi karibuni, uhusiano kati ya China na Grenada umeendelezwa kwa hatua madhubuti, huku pande hizo mbili zikitendeana kwa kuheshimiana na usawa, kuimarisha hali ya kuaminiana kisiasa, kupata matokeo yenye manufaa kwenye ushirikiano wa kivitendo katika sekta mbalimbali, na kuzidisha urafiki kati ya watu wa pande hizo mbili.

“China inapenda kufanya juhudi pamoja na Grenada katika kuimarisha ushirikiano wa mikakati ya maendeleo na kusukuma mbele maendeleo zaidi ya ushirikiano wa pande mbili ili kupata matokeo mengi ya kunufaisha vizuri zaidi watu wa pande hizo mbili” ameongeza.

Rais Xi amesema, China inaiunga mkono Grenada katika kutafuta kwa kujitawala na kujiamulia njia ya kujiendeleza ya kulingana na hali halisi ya nchi yake , na China inapenda kuimarisha mawasiliano na Grenada ya kubadilishana mawazo kuhusu uzoefu wa utawala wa nchi .

Amesema China pia inaiunga mkono Grenada katika kuongeza uwezo wake katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuzuia na kupunguza athari za maafa, na kuendelea kuongeza ufahamu wa jumuiya ya kimataifa kuhusu wasiwasi wa nchi za visiwa vidogo kuhusu mabadiliko ya tabianchi na mahitaji yao.

Kwa upande wake Waziri Mkuu Mitchell ameeleza shukrani kwa msaada wa wakati wa China baada ya Grenada kukumbwa na kimbunga kikali mwezi Julai mwaka jana.

“Katika miaka 20 iliyopita, uhusiano wa Grenada na China umeendelea kwa kina siku hadi siku, na Grenada inafuata kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja na inaamini kuwa mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi ya China lazima viheshimiwe,” Waziri Mkuu Mitchell amesema.

Waziri Mkuu Mitchell akisisitiza jukumu ongozi la China katika Nchi za Kusini, amesema Grenada itasimama kidete na China katika kutekeleza mapendekezo makuu matatu kwa Dunia na kulinda amani na utulivu wa dunia. 

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Waziri Mkuu wa Grenada Dickon Mitchell, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Januari 13, 2025. (Xinhua/Ding Lin)

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Waziri Mkuu wa Grenada Dickon Mitchell, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Januari 13, 2025. (Xinhua/Ding Lin)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha