

Lugha Nyingine
Rais Xi aagiza kufanya juhudi zote za kuwaaokoa watu walioathirika kwenye tetemeko la ukubwa wa 6.8 mkoani Xizang, China
BEIJING - Rais Xi Jinping wa China ameagiza kufanya juhudi kwa nguvu zote kuwaokoa watu walioathirika, kuwatibu watu waliojeruhiwa, na kupunguza vifo vya watu kwa kadiri iwezavyo kufuatia tetemeko la ardhi la ukubwa wa kipimo cha 6.8 ambalo limeleta madhara makubwa katika wilaya moja katika Mkoa unaojiendesha wa Xizang, kusini magharibi mwa China jana Jumanne asubuhi.
Rais Xi, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), ametoa agizo hilo muhimu, akitaka kutafuta kwa nguvu zote watu walioathirika na kuokoa na kutoa huduma za matibabu kwa majeruhi.
Pia amehimiza kufanya juhudi za kuzuia maafa mengine kutokana na tetemeko la ardhi, kuwapa makazi mapya wakazi walioathirika, na kushughulikia athari ipasavyo.
“Ni muhimu kuimarisha ufuatiliaji wa tetemeko la ardhi na tahadhari ya mapema, kutenga haraka vifaa vya misaada ya maafa, kuharakisha ukarabati wa miundombinu iliyoharibiwa, kuhakikisha mahitaji ya kimsingi ya maisha ya wakaazi yanatimizwa, na kuwahakikishia watu wote wanaishi salama na kujisitiri kwenye joto katika siku za baridi" Rais Xi amesema.
Katika maagizo yaliyotolewa siku hiyo na Waziri Mkuu wa China Li Qiang, ambaye pia ni mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC, amehimiza kufanya uchunguzi haraka juu ya hali ya maafa nahali ya watu walioathirika , kuandaa operesheni za pande zote za utafutaji na uokoaji na kupunguza vifo vya watu.
Amesema kwa vile eneo lililokumbwa na tetemeko hilo la ardhi liko katika uwanda wenye baridi kali, kila namna iwezekanayo lazima itumike ili kuhakikishia maisha ya kimsingi ya watu walioathirika na kuwasaidia kujisitiri kwenye joto wakati wa majira haya ya baridi.
Naibu Waziri Mkuu wa China, Zhang Guoqing, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC, ameongoza timu kuelekea eneo la tetemeko la ardhi ili kuelekeza kazi za uokoaji na utoaji msaada.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma