China kuwa na muundombinu ya kitaifa wa data tayari ifikapo Mwaka 2029

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 07, 2025

Mfanyakazi akikagua  uendeshaji wa vifaa katika Maabara Muhimu ya Kitaifa ya Data Kubwa ya Umma katika Chuo Kikuu cha Guizhou mjini Guiyang, Mkoa wa Guizhou, kusini-magharibi mwa China, Agosti 29, 2024. (Xinhua/Yang Wenbin)

Mfanyakazi akikagua uendeshaji wa vifaa katika Maabara Muhimu ya Kitaifa ya Data Kubwa ya Umma katika Chuo Kikuu cha Guizhou mjini Guiyang, Mkoa wa Guizhou, kusini-magharibi mwa China, Agosti 29, 2024. (Xinhua/Yang Wenbin)

BEIJING – Kamati ya Kitaifa ya Maendeleo na Mageuzi na idara nyingine mbili za China jana Jumatatu imetoa mwongozo ikisema, lengo la China ni kukamilisha ujenzi wa muundo mkuu wa miundombinu ya data za kitaifa ifikapo mwaka 2029.

Hii ni sehemu ya kazi ya nchi ya kuhimiza kujenga soko la data za kitaifa lililounganishwa na kuendeleza uchumi wa kidijitali katika sehemu nyingi zaidi nchini, mwongozo huo umedhihirisha.

Kutokana na maendeleo ya kasi ya teknolojia ya kidijitali na miundombinu yake duniani, kuendeleza miundombinu ya data za kitaifa, kumekuwa ni kujenga aina mpya ya miundombinu inayounga mkono ukusanyaji, ujumlishaji, usambazaji, uchakataji, mzunguko, matumizi, uendeshaji na usalama wa data.

Mwongozo huo umesema, maendeleo ya miundombinu ya data ya China bado yapo katika hatua za mwanzo. China inapanga kukamilisha mpango wa jumla wa utendaji wa pande mbalimbali na kwenye ngazi tofauti kuhusu ujenzi wa miundombinu ya data za kitaifa kati ya mwaka 2024 na 2026 na wakati huo huo kukamilisha mitandao ya data na vifaa vya nguvu za mifumo ya kompyuta kati ya mwaka 2027 na 2028.

Mwongozo huo umeeleza, China pia imedhamiria kuboresha mtandao wa 5G hadi daraja la 5G-A na kuhimiza utafiti, uhuishaji na uvumbuzi unaohusika na 6G.

Mtandao wa 5G-A umezidi mtandao wa sasa wa 5G kwa vigezo vya kasi, muda na utulivu, kiwango cha muunganisho na matumizi ya nishati. Unafikia kasi ya kunukuu data ya gigabiti 10 kwa sekunde na kasi ya kupeleka data ya gigabiti 1 kwa sekunde, na muunganisho wa gharama nafuu kwa Intaneti ya Vitu (IoT).

Miji ya Beijing na Shanghai na miji mingine ya China tayari imeanza kutoa huduma za mtandao wa 5G-A katika baadhi ya sehemu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha