Xi Jinping asisitiza kushinda mapambano magumu ya muda mrefu dhidi ya ufisadi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 07, 2025

Xi Jinping, Rais wa China ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akihutubia mkutano wa nne wa wajumbe wote wa kamati kuu ya 20 ya Ukaguzi wa Nidhamu ya CPC (CCDI) Januari 6, 2025 (Xinhua/Li Xueren)

BEIJING - Xi Jinping, Rais wa China ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), Jumatatu wakati akihutubia mkutano wa nne wa wajumbe wote wa kamati kuu ya 20 ya Ukaguzi wa Nidhamu ya CPC (CCDI) uliofanyika siku hiyo Beijing ametoa wito wa kushinda kithabiti mapambano hayo magumu ya muda mrefu kwa pande zote dhidi ya ufisadi, na Chama ijijenge kwa vigezo vikali na kwa moyo wa mageuzi.

Rais Xi amesema juhudi ambazo hazijawahi kushuhudiwa zimefanywa katika kujijenga kwa vigezo vikali kwa Chama na kufanya mapambano dhidi ya ufisadi tangu mwanzo wa zama mpya, zikitoa matokeo yanayotambuliwa na watu wengi.

Amesisitiza haja ya kuchukua hatua madhubuti na endelevu ili kupambana na ufisadi.

"Ufisadi ni tishio kubwa zaidi kwa Chama, na kupambana nayo kunawakilisha aina kamili ya kujifanyia mageuzi," Rais Xi amesema.

Rais Xi amesema, kikikabiliwa na changamoto kubwa katika mapambano dhidi ya ufisadi, Chama kimeendelea kuwa na dhamira ya kuchunguza na kushughulikia kesi zote za ufisadi ili kudumisha uadilifu wa maofisa.

Lakini pia amedhihirisha kuwa mapambano dhidi ya ufisadi bado ni "changamoto kubwa na ngumu," akitoa wito wa kuimarishwa kwa dhamira na imani katika suala hili.

Amesisitiza umuhimu wa kupiga hatua kubwa zaidi katika kujijenga kwa vigezo vikali kwa Chama ili kuhakikisha Chama kinaendelea kuwa muhimili imara wa uongozi katika kujenga ujamaa wenye umaalum wa China na kuhakikisha Ujenzi wa Mambo ya Kisasa wa China unaendelea kwa hatua madhubuti.

“Ni muhimu kuhimiza usimamizi wa kisiasa uendelee kwa hali halisi, kulenga kwa usahihi na kufanyika siku zote kama kawaida, na kufuata kithaibiti misimamo na sera za Kamati Kuu ya CPC kwa maneno na vitendo,” Rais Xi amesema.

Rais Xi amesisitiza kuwa kuimarisha ujenzi wa nidhamu ya chama ni kazi inayoendelea siku zote, ni lazima kuanzisha utaratibu wa elimu ya nidhamu ulio wa kudumu na wenye ufanisi wa muda mrefu, na ni muhimu kutekeleza usimamizi mkali huku kuwatia moyo menejimenti ili kuwawezesha kufuata nidhamu na sheria katika kufanya mageuzi na uvumbuzi.

Xi Jinping, Rais wa China ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akihutubia mkutano wa nne wa wajumbe wote wa kamati kuu ya 20 ya Ukaguzi wa Nidhamu ya CPC (CCDI) Januari 6, 2025 (Xinhua/Xie Huanchi)

Xi Jinping, Rais wa China ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akihutubia mkutano wa nne wa wajumbe wote wa kamati kuu ya 20 ya Ukaguzi wa Nidhamu ya CPC (CCDI) Januari 6, 2025. (Xinhua/Yue Yuewei)

Li Xi, mjumbe wa kudumu wa  Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni  katibu wa Kamati Kuu ya Ukaguzi wa Nidhamu ya CPC (CCDI), akitoa ripoti ya kazi kwa niaba ya Kamati ya Kudumu ya CCDI kwenye mkutano wa nne wa wajumbe wote wa kamati kuu ya 20 ya Ukaguzi wa Nidhamu ya CPC (CCDI) Januari 6, 2025. (Xinhua/Yue Yuewei)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha