Hotuba za Salamu za Mwaka Mpya za Rais Xi zaleta imani kwa dunia iliyopo kwenye msukosuko

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 02, 2025

Picha hii ikionyesha treni ya mwendokasi ya CR450AF mjini Beijing, China, Desemba 29, 2024. (Xinhua/Ju Huanzong)

Picha hii ikionyesha treni ya mwendokasi ya CR450AF mjini Beijing, China, Desemba 29, 2024. (Xinhua/Ju Huanzong)

BEIJING - Wataalamu wa ng'ambo wamesema, hotuba ya Salamu za Mwaka Mpya aliyotoa Rais wa China Xi Jinping siku ya Jumanne imeonyesha mafanikio dhahiri yaliyopatikana nchini China katika kutafuta maendeleo ya sifa bora katika mwaka uliopita, na hotuba yake hiyo imeleta imani kwa dunia inayokumbwa na changamoto na msukosuko.

Hotuba hiyo ya salamu za mwaka mpya aliyotoa Rais Xi pia imeonyesha wajibu wa China ikiwa nchi kubwa wa kuhimiza amani na maendeleo ya dunia, na dhamira na hatua yake ya kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja, na pia imeeleza matumaini ya kujenga kwa pamoja siku nzuri za Dunia za baadaye.

Kuingiza imani kwenye uchumi wa Dunia

"Tumefanya juhudi za kukabiliana na athari za mabadiliko ya mazingira ya ndani na nje ya nchi. Tumetoa sera zinazohusu mfumo wa kikamilifu ili kupata mafanikio halisi kwa hatua madhubuti katika kusukuma mbele maendeleo ya sifa bora. Uchumi wa China umeimarika na uko kwenye mwelekeo wa kukua," Rais Xi amesema katika hotuba yake ya salamu za Mwaka Mpya.

"Sera na hatua za pande zote za China za kukabiliana na changamoto za ndani na za kimataifa zinaonyesha uwezo wake mkubwa wa utawala na unyumbulikaji wake," amesema Benjamin Mgana, mhariri mkuu wa habari za kimataifa katika gazeti la The Guardian la Tanzania.

Kuanzia ufufukaji wa uchumi hadi uzalishaji wa magari zaidi ya milioni 10 yanayotumia nishati mpya kwa mwaka, hatua hizi muhimu zinaonyesha mafanikio ya mkakati wa maendeleo ya sifa bora wa China, Mgana amesema, akieleza kuwa, kusukuma mbele maendeleo ya kijani ya kutoa kaboni chache na kuibuka kwa viwanda vya aina mpya na miundo mipya ya biashara kunasisitiza dhamira ya China kwa maendeleo endelevu.

Kuchangia kwenye amani na maendeleo ya Dunia

"Katika dunia nzima ya kufanya mageuzi na kukumbwa na msukosuko, China ikiwa nchi kubwa inayowajibika, inafanya juhudi zaidi za kuhimiza mageuzi ya usimamizi wa Dunia na kuzidisha mshikamano na ushirikiano kati ya Nchi za Kusini," Rais Xi amesema katika hotuba yake hiyo.

"China inazidi kuwa nguvu kuu ya kuleta utulivu kwa kupitia utetezi wake wa kufanya ushirikiano wa pande nyingi na ufunguaji mlango," amesema Lyazid Benhami, naibu mwenyekiti wa Shirika la Paris la Urafiki wa Ufaransa na China.

Kwa kupitia kuhimiza mageuzi ya vyombo vya kimataifa, China itatoa sauti kwa ajili ya nchi zilizowekwa ukingoni kwa muda mrefu na kujitahidi kuhakikisha sauti zao zinasikika, Benhami ameongeza.

Kwa pamoja kujenga mustakabali bora wa baadaye

"Kwa kukabiliwa na mabadiliko ambayo hayajaonekana katika miaka 100 iliyopita, ni lazima kuondokana na mifarakano na migogoro kwa maono mapana, na kuwa na uchangamfu mkubwa kwa kufuatilia mustakabali wa binadamu," rais Xi amesisitiza katika hotuba yake ya salamu za mwaka mpya, akiongeza kuwa China itajiunga pamoja na nchi zote katika kuhimiza urafiki na ushirikiano, kuongeza hali ya kufundishana kati ya tamaduni mbalimbali, na kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

"Lazima kwa pamoja tujenge mustakabali bora wa dunia," Rais Xi ametoa wito huo.

Gan Tian Loo, naibu mwenyekiti wa Shirika la Mawasiliano ya Malaysia na China, amesema kuwa pendekezo la kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja linachangia kuhimiza ujenzi wa mambo ya kisasa wa Dunia, kwenda zaidi ya migogoro na mapambano, kuhimiza maendeleo ya amani, kufanya ushirikiano wa kunufaishana badala ya mchezo wa kutiana hasara, na kwa kupitia kufanya mawasiliano na kuongeza maelewano kwa kuzuia migongano ya kistaarabu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha