Xi asisitiza kujiamini na kufanya kazi kwa bidii katika mwaka 2025 ili kuondokana na changamoto

(CRI Online) Januari 01, 2025

Rais Xi Jinping wa China ametoa wito kwa nchi ya China kuendelea kujiamini katika mwaka 2025, akisema China ni nchi ya pili kwa uchumi mkubwa duniani inaweza kushinda changamoto na shinikizo kwa kufanya kazi kwa bidii.

Xi aliyasema hayo jana siku ya Jumanne katika salamu zake za mwaka mpya wa 2025 alizotoa kupitia Shirika Kuu la Utangazji la China CMG na mtandao wa internet. Ameeleza kuwa ikiwa inadhamiria kukamilisha kabisa Mpango wake wa 14 wa Miaka Mitano katika mwaka 2025, China itatekeleza sera kwa makini zaidi na kwa hatua madhubuti, kuweka kipaumbele kwenye maendeleo ya hali ya juu, kuhimiza kujitegemea zaidi na kujiimarisha katika sayansi na teknolojia, na kudumisha kasi nzuri katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Rais Xi pia aliapa kuendeleza mageuzi nchini, akitaja mkutano wa Chama uliofanyika mwezi Julai ambao ulipitisha mpango mkuu wa mageuzi. Waraka kwenye mkutano huo ulielezea kazi muhimu za mageuzi kwa miaka mitano ijayo na kupendekeza zaidi ya mipango mikuu 300 ya mageuzi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha