

Lugha Nyingine
China yatoa ripoti ya kwanza kuhusu utafiti wa kisayansi katika kituo cha anga ya juu
Picha hii ya skrini iliyopigwa katika Kituo cha Udhibiti wa Anga cha Beijing Desemba 17, 2024 ikionyesha wanaanga wa chombo cha Shenzhou-19 Cai Xuzhe (juu) na Song Lingdong (chini) wakifanya kazi nje na ndani ya lango la kufunga kwa juu la kituo cha anga ya juu cha China. (Xinhua/Li Jie)
BEIJING - China imetoa ripoti yake ya kwanza inayoelezea maendeleo yaliyopatikana katika utafiti wa kisayansi na matumizi yanayohusiana na kituo cha anga ya juu cha nchi hiyo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita ambapo Shirika la Anga ya Juu la China (CMSA), ambalo limeandaa ripoti hiyo "kuadhimisha miaka miwili tangu kuanzishwa kikamilifu kwa kituo hicho," limesema kuwa ripoti hiyo itakuwa ikitolewa kila mwaka kutokana na maendeleo ya majukumu ya anga ya juu yanayoendelea.
Ripoti hiyo, iliyotolewa jana Jumatatu, inajikita katika maeneo kama vile maisha ya anga ya juu na utafiti wa binadamu, sayansi ya maumbile ya mikrograviti, na teknolojia mpya za anga ya juu na matumizi.
Inaangazia matokeo 34 wakilishi ya utafiti wa kisayansi na matumizi yaliyochaguliwa kutoka kwenye sampuli zilizorejeshwa hapo awali, data ya utafiti, majaribio ya ndani ya obiti, na maendeleo muhimu katika miradi ya kisayansi na matumizi, vilevile shughuli mbalimbali za kueneza sayansi, ikionyesha uwezo na moyo wa ubunifu wa China katika nyanja ya teknolojia ya anga ya juu, kwa mujibu wa CMSA.
Kati ya matokeo hayo wakilishi, 13 yanahusiana na maisha ya anga na utafiti wa binadamu, 12 yanahusiana na utafiti wa sayansi ya maumbile ya mikrograviti, na tisa yanahusiana na teknolojia mpya ya anga ya juu na utafiti wa matumizi.
Kundi la awali la majaribio ya sayansi ya anga ya juu, miradi ya matumizi, na majaribio ya teknolojia ndani ya kituo hicho cha anga ya juu yameendelea vizuri, yakitoa matokeo muhimu, CMSA imebainisha.
Kuanzia Desemba 1, miradi ya kisayansi na matumizi jumla ya 181 imetekelezwa katika obiti, huku tani karibu mbili za nyenzo za kisayansi zikiwa zimewasilishwa na aina karibu 100 za sampuli za majaribio zikiwa zimerejeshwa, zikitoa terabytes zaidi ya 300 za data ya kisayansi.
Mafanikio makubwa muhimu yanajumuisha rasilimali za kwanza duniani za mchele na chembechembe za mchele wa ratoon zilizokuzwa kwenye anga ya juu, na seli za shina za kiinitete cha binadamu za kwanza zinazotofautishwa katika shina/seli ya hematopoietic katika anga ya juu.
Kituo cha anga ya juu cha China kiliingia katika hatua ya matumizi na uendelezaji wake Desemba. 31, 2022. Kwa sasa, kinafanya kazi kwa utulivu na kuonyesha ufanisi mkubwa, CMSA imeeleza.
Watafiti wakichunguza sampuli za majaribio za kituo cha anga ya juu zilizoletwa duniani na chombo cha anga ya juu cha Shenzhou-18 katika Kituo cha Teknolojia na Uhandisi wa Matumizi ya Anga ya Juu chini ya Akademia ya Sayansi ya China mjini Beijing, mji mkuu wa China, Novemba 4, 2024. (Kituo cha Teknolojia na Uhandisi wa Matumizi ya Anga ya Juu chini ya Akademia ya Sayansi ya China / kupitia Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma