

Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping atuma salamu za rambirambi kwa Kaimu Rais wa Jamhuri ya Korea kutokana na ajali ya ndege
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 30, 2024
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ametuma salamu za rambirambi kwa Kaimu Rais wa Jamhuri ya Korea Choi Sang-mok kufuatia ajali ya ndege ya abiria ya Shirika la Ndege la Jeju Air iliyosababisha vifo vya watu wengi pamoja na majeruhi.
Katika salamu hizo za rambirambi zilizotolewa jana Jumapili, Rais Xi amesema ameshtushwa kujua kwamba ajali hiyo imesababisha vifo vya watu wengi. Akiwa kwa niaba ya serikali na wananchi wa China, ametoa rambirambi za kuguswa sana kwa watu waliofariki katika ajali hiyo, na kutoa pole za dhati kwa familia zilizofiwa, na kuwatakia majeruhi wapone mapema.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma