

Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping atuma rambirambi kufuatia ajali ya ndege ya shirika la ndege la Azerbaijan
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 27, 2024
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ametuma rambirambi kwa Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev, Rais wa Russia Vladimir Putin na Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev kutokana na vifo na majeruhi katika ajali ya ndege ya Shirika la Ndege la Azerbaijan.
Kwenye rambirambi hizo zilizotumwa jana Alhamisi, Rais Xi amesema kuwa ameshtushwa kujua kwamba ndege ya abiria ya Shirika la Ndege la Azerbaijan imeanguka, ikisababisha vifo na majeruhi.
Rais Xi akiwa kwa niaba ya serikali na wananchi wa China, anaomboleza sana watu waliofariki, pia ametoa pole kwa familia zilizofiwa na kuwatakia majeruhi wapone haraka.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma