Rais Xi Jinping atoa amri ya kumpandisha cheo kamanda wa kijeshi kuwa jenerali

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 24, 2024

Xi Jinping, Rais wa China ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akikabidhi cheti cha amri ya kumpandisha   cheo kamanda wa Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) Chen Hui kuwa jenerali, katika hafla ya upandishaji cheo iliyofanyika Beijing, China , Desemba 23, 2024. (Xinhua/Li Gang)

Xi Jinping, Rais wa China ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akikabidhi cheti cha amri ya kumpandisha cheo kamanda wa Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) Chen Hui kuwa jenerali, katika hafla ya upandishaji cheo iliyofanyika Beijing, China, Desemba 23, 2024. (Xinhua/Li Gang)

BEIJING – Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), amempa cheti cha amri ya kumpandisha cheo kamanda wa kijeshi kuwa jenerali jana Jumatatu, kamanda huyo aliyepandishwa cheo ni kamanda kamisaa wa kisiasa wa vikosi vya nchi kavu vya Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA), Chen Hui.

Zhang Youxia, naibu mwenyekiti wa CMC, alitangaza amri hiyo ya kupandisha cheo, ambayo ilitiwa saini na Rais Xi, katika hafla ya upandishaji huo wa cheo iliyofanyika Beijing huku naibu mwenyekiti mwingine wa CMC, akiongoza hafla hiyo.

Rais Xi alitoa pongezi kwa jenerali huyo.

Cheo cha Jenerali ni daraja la juu zaidi kwa maafisa wa kijeshi ambao bado wako katika utumishi nchini China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha