China yapinga Marekani kuiuzia Taiwan silaha

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 23, 2024

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China amesema, hatua ya Marekani kuiuzia Taiwan silaha imekiuka sera ya kuwepo kwa China moja, na Taarifa tatu za pamoja kati ya China na Marekani na imeingilia mamlaka na maslahi ya usalama ya China.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kuhusu hatua hiyo ya Marekani, msemaji huo amesema, kitendo hicho pia kinakiuka ahadi ya viongozi wa Marekani kuhusu kutounga mkono“Taiwan kujitenga na China” na kimetoa ishara ya makosa kwa makundi ya watu wa Taiwan wanaotaka kujitenga na China.

“China inapinga hatua hiyo na imetoa malalamiko kwa Marekani” amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha