Rais Xi Jinping ashiriki na kutoa hotuba kwenye tafrija ya kumkaribisha iliyoandaliwa na serikali ya Mkoa wa Utawala Maalum wa Macao

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 20, 2024

Rais Xi Jinping akishiriki na kutoa hotuba kwenye tafrija ya kumkaribisha iliyoandaliwa na serikali ya Mkoa wa Utawala Maalum wa Macao Desemba 19 2024. (Xinhua/Ju Peng)

Rais Xi Jinping akishiriki na kutoa hotuba kwenye tafrija ya kumkaribisha iliyoandaliwa na serikali ya Mkoa wa Utawala Maalum wa Macao Desemba 19 2024. (Xinhua/Ju Peng)

Rais Xi Jinping alishiriki na kutoa hotuba kwenye tafrija ya kumkaribisha iliyoandaliwa na serikali ya Mkoa wa Utawala Maalum wa Macao tarehe 19. Xi Jinping alieleza kuwa miaka mitano iliyopita ni miaka yenye hali isiyo ya kawaida katika historia ya Macao, ni miaka iliyokabiliana na mabadiliko ya kasi zaidi ambayo hayajaonekana katika miaka mia moja iliyopita, na pia ni ya kujaribiwa katika janga kubwa la UVIKO-19, serikali ya awamu ya tano ya mkoa wa utawala maalumu wa Macao imeungana na kuongoza watu wa sekta zote za jamii ya Macao kukabiliana na matatizo na kuchukua hatua halisi za kushinda taabu, kuhimiza ukuaji wa uchumi kuendelea kurejea katika hali nzuri, na shughuli mbalimbali zimepata maendeleo makubwa sana, na kuandika ukurasa mpya wa mafanikio ya Macao katika uzoefu wa "nchi moja, mifumo miwili".

Cai Qi, Li Hongzhong, He Weidong, He Lifeng, Wang Xiaohong, Wang Dongfeng, na Xia Baolong walishiriki kwenye tafrija hiyo.  

Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China Ho Hau Wah, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong John Lee, Mtendaji Mkuu mteule wa Mkoa wa Utawala Maalum wa Macao Sam Hou Fai, Mtendaji Mkuu wa zamani Chui Sai On, maofisa wakuu wa serikali ya Mkoa Maalum wa Utawala wa Macao, na wajumbe wa sekta mbalimbali wa Macao pia walishiriki kwenye tafrija hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha