China yafanya Mkutano wa Kamati Kuu ya Kazi ya Uchumi kupanga mipango ya Mwaka 2025

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 13, 2024

Xi Jinping, Rais wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitoa hotuba muhimu kwenye Mkutano wa mwaka wa Kamati Kuu ya Kazi ya Uchumi uliofanyika Beijing, mji mkuu wa China. (Xinhua/Xie Huanchi)

BEIJING - Mkutano wa mwaka wa Kamati Kuu ya Kazi ya Uchumi umefanyika Beijing kuanzia Jumatano hadi Alhamisi, ambapo viongozi wa China wameamua kazi muhimu za uchumi za Mwaka 2025, na rais Xi Jinping ametoa hotuba muhimu kwenye mkutano huo.

Katika hotuba yake hiyo, Rais Xi amekumbuka kazi ya uchumi ya China katika mwaka 2024, kuchambua hali ya hivi sasa ya uchumi na kupanga kazi ya kiuchumi ya mwaka ujao.

Mkutano huo umedhihirisha kuwa uchumi wa China umeendelea kwa utulivu kwa ujumla, umepata maendeleo ya sifa bora kwa hatua madhubuti mwaka 2024, na malengo na majukumu makuu ya mwaka ya maendeleo ya uchumi na jamii yanatazamiwa kukamilika kwa mafanikio.

Mkutano huo umesema, mchakato wa maendeleo katika mwaka uliopita ulikuwa wa hali isiyo ya kawaida, na mafanikio yaliyopatikana yanawatia watu moyo. Ripoti ya mkutnao imeeleza kuwa sera mfululizo za nyongeza zilizotolewa na uongozi wa CPC mwishoni mwa Septemba zimeongeza kwa ufanisi imani ya jamii na kusababisha kuimarika dhahiri kwa uchumi.

Huku mkutano huo ukitambua athari mbalimbali zinazozidi kuonekana kutokana na mabadiliko katika mazingira ya nje na mambo magumu na changamoto nyingi ambazo bado zinakabili uendeshaji wa uchumi wa China kwa hivi sasa, mkutano huo umeeleza kuwa mazingira ya uungaji mkono na mwelekeo wa kimsingi wa maendeleo ya muda mrefu ya uchumi wa China bado haujabadilika.

"Ni lazima tukabiliane na mambo magumu, tuimarishe imani yetu, na kujitahidi kuzifanya juhudi zote kuwa mafanikio halisi katika maendeleo," mkutano huo umesema.

Mkutano huo umesema, ni lazima kutekeleza sera za uchumi wa jumla zinazoweza kuhimiza juhudi na zenye matokeo zaidi, kudumisha mwelekeo wa kukua kwa uchumi, ili kutimiza malengo na majukumu katika Mpango 14 wa Maendeleo ya Uchumi na Jamii ya Miaka Mitano (2021-2025) kwa sifa bora na kuweka msingi thabiti wa mwanzo mzuri kwa Mpango wa 15 wa Maendeleo ya Uchumi na Jamii Miaka Mitano (2026-2030), mkutano huo umesema.

Kwa mwaka ujao, mkutano huo umesisitiza haja ya kudumisha ukuaji tulivu wa uchumi, kudumisha hali ya utulivu ya jumla ya utoaji nafasi za ajira na bei za vitu, kuhakikisha uwiano wa kimsingi kati ya mapato na matumizi ya kimataifa , na kuongeza mapato ya wakazi sambamba na ukuaji wa uchumi.

Wajumbe wa kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang na Li Xi wamehudhuria mkutano huo.

Li Qiang ametoa hotuba ya kuhitimisha, akitoa matakwa ya kutekeleza kanuni elekezi za hotuba muhimu ya Rais Xi na kufanya vizuri kazi ya uchumi ya mwaka ujao.

Xi Jinping, Rais wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitoa hotuba muhimu katika Mkutano wa mwaka wa Kamati Kuu wa Kazi ya Uchumi uliofanyika Beijing, mji mkuu wa China. (Xinhua/Xie Huanchi)

Xi Jinping, Rais wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitoa hotuba muhimu kwenye Mkutano wa mwaka wa Kamati Kuu wa Kazi ya Uchumi uliofanyika Beijing, mji mkuu wa China. (Xinhua/Ju Peng)

Li Qiang, Waziri Mkuu wa China ambaye pia ni mjumbe wa kudumu wa  Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akitoa hotuba kwenye Mkutano wa mwaka wa Kamati Kuu ya Kazi ya Uchumi uliofanyika Beijing . (Xinhua/Xie Huanchi)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha