Rais Xi Jinping wa China atoa pongezi kwa Rais Mteule wa Ghana John Dramani Mahama

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 12, 2024

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ametuma salamu za pongezi kwa John Dramani Mahama siku ya Jumatano kwa kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Ghana.

Huku akisema kuwa Ghana ni moja kati ya nchi za kwanza za Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na China na pia ni mshirika muhimu wa kimkakati wa China barani Afrika, Rais Xi amesema urafiki kati ya China na Ghana una historia ndefu na umekuwa ukiimarishwa muda baada ya muda.

Katika miaka ya hivi karibuni, uhusiano wa pande mbili umefurahia mwenendo mzuri wa maendeleo, huku kukiwa na ushirikiano wa manufaa yenye matunda halisi katika sekta mbalimbali, Rais Xi amesema.

Pia katika salamu zake, Rais Xi amesema kutilia maanani sana maendeleo ya uhusiano kati ya China na Ghana na anapenda kushirikiana na Rais Mteule Mahama kuenzi urafiki wa jadi, kuzidisha hali ya kuaminiana kisiasa, na kuhimiza uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kati ya China na Ghana uendelezwe kwa kina na kupata matokeo halisi, ili kuleta manufaa zaidi kwa watu wa nchi hizo mbili. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha