

Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping asema China itaendelea kuwa injini kubwa zaidi ya ukuaji wa uchumi duniani
Rais Xi Jinping wa China akikutana na wakuu wa mashirika makubwa ya uchumi ya kimataifa waliokuja Beijing kushiriki kwenye Mazungumzo ya "1+10", katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Desemba 10, 2024. (Xinhua/Huang Jingwen)
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping siku ya Jumanne alipokutana na wakuu wa mashirika makubwa ya uchumi ya kimataifa, ambao walikuwa Beijing kushiriki kwenye mazungumzo ya "1+10" alisema China inajaa imani ya kufikia lengo la ukuaji wa uchumi la mwaka huu na itaendelea kufanya kazi yake ya kuwa injini kubwa ya ukuaji wa uchumi wa dunia.
Viongozi hao ni pamoja na Mkuu wa Benki Mpya ya Maendeleo Dilma Rousseff, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa Kristalina Georgieva, Mkuu wa Kundi la Benki ya Dunia Ajay Banga, na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani Ngozi Okonjo-Iweala.
Ukuaji wa China
Rais Xi amewajulisha wageni hao kuhusu mkutano wa tatu wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), hasa hatua muhimu zilizochukuliwa hivi karibuni na China. Amesema baada ya maendeleo endelevu na ya kasi katika zaidi ya miaka 40 iliyopita, uchumi wa China umeingia katika kipindi cha maendeleo ya sifa bora, ikichangia karibu asilimia 30 katika ukuaji wa uchumi wa Dunia.
China itafungua zaidi mlango kwa nje, kuziwezesha kanuni zake kuunganishwa na kanuni za kimataifa za uchumi na biashara zenye vigezo vya juu, na kujenga mazingira ya biashara ya soko huria, kufuata sheria na ya kimataifa ili kutoa fursa zaidi kwa nchi mbalimbali na kunufaika pamoja na faida zaidi ya maendeleo amesema.
Hamasa ya China
Wageni hao kutoka nchi za nje wamepongeza mafanikio makubwa ya China, hususan katika kupunguza umaskini na kuhimiza ujengaji wa nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora, wakisema mawazo ya maendeleo ya China yanayoweka kipaumbele cha juu kwa watu yamepata mafanikio na kufuata hali halisi, na yametoa ufunuo kwa Dunia.
Wamesema China imeendelea kuzidisha mageuzi kwa kina, kupanua ufunguaji mlango na kufikia maendeleo ya sifa bora, ikitoa fursa kubwa kwa Dunia, hasa nchi za Kusini.
Wameeleza kuwa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI), Pendekezo la Maendeleo ya Dunia, Pendekezo la Usalama wa Dunia na Pendekezo la Ustaarabu wa Dunia yameonyesha vya kutosha kazi ya China ikiwa nchi kubwa inayowajibika na kutoa jukwaa muhimu kwa nchi za Kusini kufikia maendeleo yao zenyewe.
Rais Xi Jinping wa China akikutana na wakuu wa mashirika makubwa ya kimataifa ya kiuchumi, waliokuja Beijing kushiriki kwenye Mazungumzo ya "1+10", katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Desemba 10, 2024. (Xinhua/Zhai Jianlan)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma