

Lugha Nyingine
Mkutano wa biashara ya umeme Afrika Mashariki wafunguliwa nchini Kenya ili kuimarisha usalama wa nishati
Mkutano wa Biashara ya Kuzalisha Umeme kwa Bwawa la Maji Afrika Mashariki 2024 (EAPP) unaofanyika kwa siku tatu umeanza Jumatatu mjini Mombasa nchini Kenya katika juhudi za kuimarisha usalama wa nishati katika kanda hiyo.
Mkutano huo ulioandaliwa na EAPP, shirika la kikanda linalolenga kuhimiza na kuwezesha ushirikiano katika nyanja ya uzalishaji na usambazaji wa umeme, kwa ushirikiano na Benki ya Dunia, unawaleta pamoja wajumbe zaidi ya 300 wakiwemo mawaziri wa nishati, waendeshaji, mashirika ya huduma, wataalam wa kimataifa, na washirika wa maendeleo kutoka kote barani Afrika kujadili mikakati ya ushirikiano wa nishati.
Katika hotuba yake ya ufunguzi, Waziri wa Nishati na Petroli wa Kenya, Opiyo Wandayi, amesema hatua kubwa zinaonekana katika maendeleo ya miundombinu ya kikanda ya umeme katika nchi zinazounganishwa ili kuruhusu biashara baina ya nchi mbili na soko kuu la ushindani.
Naye mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la EAPP na waziri wa nishati wa Uganda, Okaasai Opolot, amesema miundombinu ya pamoja kati ya masoko ya nchi wanachama wa EAPP itafanya nishati iwe bei ya chini na ujumuishaji wa nishati mbadala inayozalishwa katika nchi wanachama.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma